Shaidi kesi ya Lema adaiwa kuiongopea Mahakama

Mbunge wa Arusha Godbless Lema

Na Mwandishi Wetu, Arusha

SHAHIDI wa sita katika kesi ya kupinga matokeo ya Mbunge wa Arusha
Mjini (CHADEMA) Godbless Lema, Said Athumani amedaiwa kutoa ushahidi wa
uongo mahakamani leo. Mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Gabriel Rwakibarila, Wakili anayemtetea Lema katika shauri hilo Method Kimomogoro jana aliieleza mahakama kuwa shahidi huyo ametoa ushahidi
wa uongo mahakamani.

Akimhoji shahidi huyo Kimomogoro alimtaka shahidi huyo kuieleza
Mahakama wakati wa kampeni alihudhuria miktano mingapi nay a vyama
ganai ambapo shahidi huyo aliieleza mahakama kuwa alihudhuria mikutano
mitatu ya Vyama vya CCM, Chadema na TLP iliyofanyika katika eneo la kwa
Mrombo, kata ya Terrat, mikutano ambayo alidai ilifanyika kwa siku
tofauti mwezi Agosti 2010.

Shahidi huyo alidaiwa kutoa ushahidi wa uongo baada ya kuieleza
mahakama kuwa CCM na TLP ilifanya mikutano ya kampeni katika eneo la
kwa Mrombo, mwezi wa Agosti jambo ambalo Kimomogoro aliieleza mahakama
hiyo kuwa vyama hivyo havikuwahi kufanya mikutano ya kampeni katika
eneo hilo mwezi Agosti.

Mahojiano baina ya wakili Kimomogoro na shahidi huyo yalikuwa kama ifuatavyo; Wakili: Wakati wa kampeni ulikuwa na tabia ya kusoma
magazeti, kusikiliza redio au huwa una tabia ya kuangalia TV?
Shahidi:Siyo mara kwa mara ni mara chache sana.

Wakili: Mkutano wa CCM ulifanyika tarehe ngapi?
Shahidi; sikumbuki tarehe
Wakili: Wewe ni mwanachama wa Chadema?
Shahidi: Hapana
Wakili: Kwani unakumbuka siku ya mkutano wa Chadema lakini wa CCM na
Chadema huwezi hata kukisia,Chadema inakuvutia?
Shahidi: Ni miongoni mwa vyama vya siasa vyenye nguvu
Wakili: Ni lini uliitwa mara ya kwanza kutoa ushahidi hapa Mahakamani
Shahidi: Ni mwanzoni mwa mwezi wa 11,2010 nilihitajika kwenda kutoa
maelezo niliyoyasikia kwenye mkutano huo kwa Wakili Modest Akida na
aliniambia nikatoe maelezo niliyoyasikia kwenye mkutano wa Chadema
uliofanyika kwa mrombo na siyo wa Chadema wala TLP
Wakili: Naomba nikuite mwongo, unafahamu CCM, TLP haikuwahi kufanya
mikutano kwa Mrombo mwezi wa nane, nani alikwambia maelezo haya?
Shahidi: Si kweli ila tarehe sikumbuki
Awali akiongozwa na wakili wa utetezi Modest Akida, shahidi huyo
aliieleza Mahakama kuwa wakati Lema akijinadi kwa wapiga kura hao
alidai kuwa wapiga kura hao wafanye chaguo sahihi, wasije wakawachagua
watu ambao ni sawa sawa na wapiti njia kama aliyekuwa Mgombea wa CCM
Dk. Batilda Buriani kwa sababu kwa mila na desturi za wachaga na
wamasai haziruhusu kuongozwa na mwanamke..

“Wananchi angalieni sana hawa wanawake wanaojifunga vilemba, mkimchagua mtakuwa mnakaribisha Ma-Alqaeda, Huyu mama alisema endapo atashinda kwatika uchaguzi huu, ataifunga kituo cha redio cha Safina (ya Kikristo) kwa madai kuwa ilikuwa inampa Lema alikuwa akipewa vipindi kwa ajili ya kunadi sera zake,” alidai shahidi huyo akimnukuu Lema.

Aliongeza kuwa Lema aliwaeleza wananchi hao kuwa Dk.Batilda alikuwa na
mimba hivyo wananchi wampe mimba ya pili kw akuhakikisha kuwa
anashindwa siku matokeo ya uchaguzi yatakapotangazwa,kwa hiyo wananchi
hao wampigie kura kwani yeye ndiye mbunge sahihi wa Arusha Mjini.

Akiendelea kuhojiwa na Kimomogoro, shahidi huyo alidai kuwa maneno hayo
yaliyotolewa na Lema dhidi ya Batilda, yalimuudhi kwani watanzania
tumelelewa katika maadili ya kutobaguana kidini wala kikabila.

Aidha wakili Kimomogoro aliiomba mahakaa kumuonyesha shahidi huyo
nakala ya gazeti la Mtanzania toleo namba 5229 la Septemba 8, 2010
ambalo lilikuwa na kichwa kinachosema “DK BURIANI AWEKA MAMBO
HADHARANI”, nakala ambayo shahidi huyo alisoma baadhi ya vipengele
katika taarifa hiyo.

“sumu ya udini na ukabila imemagwa ndani ya jimbo la Arusha” moja ya
kipengele alichokisoma shahidi huyo.

Wakili: Kulingana na taarifa uliyosoma ni kweli masula ya udini na
ukabila yalikuwa yameanzishwa na wanachama wa CCM?
Shahidi: Ndiyo
Shauri hilo limeahirishwa hadi kesho ambapo shahidi wa saba anatarajiwa
kutoa ushahidi wake.