Na mwandishi wetu Arusha
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ametoa changamoto kwa mabenki na taasisi nyingine za fedha Afrika Mashariki kuongeza nafasi za mikopo kwa wanawake ili kuwawezesha kuendesha biashara kubwa katika kanda hiyo.
‘’Natoa wito kwa mabenki na taasisi za fedha katika kanda hii ikiwa ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki kuwa wabunifu wakati wote.Hawana budi kutoa bidhaa na huduma mpya ambazo zitaongeza nafasi zaidi kwa wanawake kujipatia mikopo katika vikundi rasmi na taasisi za kuweka na kukopa ambazo zitawezesha wanawake kuendesha biashara kubwa na siyo tu zile ndogondogo peke yake,’’ alisema Dk. Sezibera.
Katibu Mkuu huyo wa EAC, alikuwa anazindua Jukwaa la Biashara la Wanawake Afrika Mashariki (EAWiBP) mjini Arusha, Alhamisi.
Jukwaa hilo jipya linalenga kuhamasisha ushiriki zaidi wa wanawake katika biashara na mtangamano wa Afrika Mashariki.
Dk. Sezibera alisema ingawaje EAC imejikiti katika usawa wa jinsia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwamba ni ya msingi na muhimu’’ wanawake bado wanaendelea kupata nafasi chache na kuendelea kupata shida kwa kupewa fursa chache za rasilimali katika sekta nyingi hususan ni katika maendeleoa ya kilimo na biashara.’’
Alisema ni dhana potofu kufikiria kwamba wanawake wanastahili kujikita katika biashara ndogondogo na za kati zisizorasmi pekee huku bishara kubwa ni stahili za wanaume tu.
‘’Hii ni hali ya kujirudisha nyuma na inaweza kuongeza zaidi aina mpya ya kuwabagua zaidi wanawake,’’ alisisitiza Katibu Mkuu huyo wa EAC.
Utafiti umeonyesha kwamba wakati asilimia 48 ya biashara ndogondogo kwa nchi za Kusini mwa Afrika chini ya jangwa la Sahara zinamilikiwa na wanawake, ni asilimia saba tu ndizo zinaweza kupata mikopo.
Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Jinsia wa EAC, Pepertue Miganda amebainisha kwamba changamoto wanazokabiliana nazo wanawake katika kujitafutia maendeleo ya kijamii na kiuchumi zinatokana na ukosefu wa taarifa za sera na biashara zinazowahusu wanawake moja kwa moja.
Kuanzishwa kwa jukwaa hilo la biashara kwa wanawake wa kanda hii kumetokana na wazo lilitolewa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) kwa kuungwa mkono na taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) kwa lengo la kuweka chombo kitakachoshughulikia changamoto wanazokabili biashara zinazomilikiwa na wanawake ndani ya kanda