Na Kibada Kibada – Katavi
SERIKALI imesema haitasita kuwafutia uraia wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania kutoka makazi ya wakimbizi ya Katumba Mishamo na Ulyankulu pindi watakapokiuka kufuata sheria za nchi na kwenda kinyuma na Katiba ya nchi inavyosema. Kauli hiyo ilitolewa na Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Silima Pereira wakati akiongea na wakimbizi waliopewa uraia kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba kwa niaba ya wakimbizi wote waliopatiwa uraia na serikali ya Tanzania baada ya taratibu kukamilika za kuwapatia uraia kwa mjibu wa sheria za nchi.
Naibu Waziri Pereira amesema Katiba inaruhusu kuwapokonya uria wale wote watakaokiuka Katiba ya Nchi watapokonywa uraia, na yeyote atakayevunja sheria anaweza kupokonywa na akipokonywa atakuwa hana Taifa kwa kuwa utaifa wa awali aliisha uvua iwapo atapokonywa uraia huo atakuwa hana utaifa la kukimbilia na ukimbizi nao atakuwa hanao pia.
Akaongeza kuwa wakimbizi waliopewa uraia watakuwa na Haki zote za msingi zilizoko kwenye katiba ikiwa ni pamoja na kuchaguliwa kuwa viongozi na kuchagua viongozi kama ilivyo kwa watanzani wenyeji. Amesema watakuwa na haki zote za kitaifa kama walivyo wenyeji na kikomo cha kutekeleza mambo haya ni mbigu.na kuongeza kuwa Fursa iliyopatikana ni muhimu sana na ni namna gani watakavyoweza kuitumia.
Akawaambia kuwa utanzania huu mpya waliopata usaidie kuijenga Tanzania isiyokuwa na mapigano,ugomvi chuki na mizozo ya namna yeyote bali iwe Tanzania ya Neema na Amani. Wakimbizi waliopewa uraia ni wale walikimbia mwaka 1972 na kuja nchini kwa kukimbia migogoro kwenye nchi yao ya Burundi na wameishi nchini zaidi ya miaka 30 kwenye makazi ya Katumba na Mishamo Mkoani Katavi na wale wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi Ulyankulu Mkoani Tabora.
Awali Mkuu wa Makazi ya Wakimbizi Katumba Athmani Igwe alieleza kuwa zoezi hili lilianza tangu mwaka 2008 kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzani,Shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa Mataifa UNHCR na Serikali ya Burundi kwa kufanya zoezi la uandikishaji wakimbizi wale waliotaka kurejea makwao waliotaka kubaki kuwa raia na kama watakuwa wamekidhi vigezo walijiandikisha na kufanyiwa taratibu zote za kisheria na wale waliokidhi vigezo ndio waliobahatika kupata uraia.
Igwe alieleza kuwa katika zoezi hilo kwenye Makazi ya Katumba watakaopewa uraia ni 62544 na kati yao 3503 wamepatiwa uraia na zoezi linaendelea. Kwa upande wa Makazi ya Mishamo na Ulyankulu zoezi la kugawa vyeti linaanza zoezi mwezi Januari mwaka 2015.na zoezi linaendelea.
Kwa upande wake Mwakilishili Mkazi wa Shilika la kuhudumia wakimbizi Nchini Tanzania Joyce Mends –Cole ameeleza kuwa UNHCR Itasaidia kuhakikisha inawatengenezea na kuwajengea miiundo mbinu ya maji, barabara, elimu, Afya na Huduma nyingine za Kijamii. Akasema shirika la kuhudumia wakimbizi kwa kusaidia na na serikali ya Tanzania ,Wahisani wa Maendeleo na wadau wengine watasaidia kwa njia moja au nyingine kuhakikisha wanasaidiwa.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Zamani wa Katavi Dk. Rajabu Rutengwe aliyehamishamiwa Mkoani Morogoro alisema wakati alipohamia Mkoa wa Katavi alikuja akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na kisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi baadaya ya Kuteuliwa na Rais na amekuwa na wakimbizi hao ambao wamepatiwa uraia mpya ambao ameishi na kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Akaongeza kuwa watu hawa ni wachapakazi kweli kweli na fursa waliyopata wataitumia kuhakikisha wanasukuma maendeleo ya mkoa na Taifa kwa ujumla akawataka wampatie ushirikiano wa Karibu Mkuu wa Mkoa mpaya Dk. Msengi kama ule waliokuwa wakimpatia wakati akiwa mkuu wa Mkoa wa Katavi kabal ya kuondoka pia akwawribisha kwenye mkoa wake mpya maandamu wafuate taratibu zote zinazotakiwa kwa mjibu wa Sheria za nchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi akiongea na wakimbizi hao aliwatakata kutumia fursa waliyopata kuujenga mkoa wa Katavi na Tanzania kwa ujumla kwa kutumia rasilimali na fursa zilizopo katika Mkoa huo.