Serikali Yatenga Fedha Kununua mashine Mpya ya CT- Scan Muhimbili.

Na Immaculate Makilika- Dodoma
SERIKALI  imeeleza kwamba Wizara ya Afya   ika mwaka wa fedha  wa 2013/2014  kwa ajili ya kununua mashine mpya ya  CT- Scan ya kisasa zaidi na yenye  uwezo mkubwa(250 slices) ili kuimarisha huduma  katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).
Aidha Serikali imefafanua katika mwaka 2012/2013 mashine ya CT- Scan ya MNH, ilikuwa imeharibika kwa takriban miezi 11,hali iliyosababisha  kuwepo kwa mrundikano wa wagonjwa waliohitaji huduma ya kipimo  cha CT-Scan.
Hayo yalisemwa  na Naibu  Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif  Rashid alipokuwa akijibu swali la Mussa Zungu(CCM)  alilouliza   kwa niaba ya  Al- Shaymaa Kwegyir(Viti Maalum –CCM)  kwamba je,ni kwanini imechukua muda mrefu kushughulikia tatizo  linalowaumiza  Watanzania ambao ni wanyonge  na wanaolazimika kutoa gharama kubwa kwa ajili ya kipimo hicho.
Naibu Waziri wa  huyo alisema ni  kweli kwamba  kutokana na ubovu wa mashine hiyo,baadhi ya wagonjwa walilazimika kutafuta huduma ya kipimo nje ya MN H ,ambapo gharama za kipimo  ni kati ya sh.200,000/= hadi 300,000/= .Serikali imesikitishwa na adha waliyopata wananchi  waliohitaji huduma hii na kushindwa kuipata.
Hata hivyo Dk. Rashid  alisema  matengenezo  ya CT-Scan  yalichukua muda mrefu  kutokana na kwamba kampuni ya Philips  Medical  Services (PMS), ambayo  ndio yenye mkataba wa matengenezo ya mashine  za X-ray  ikiwemo mashine  ya CT- Scan,kulazimika kuagiza vipuri  nje ya nchi  kwa ajili ya matengenezo  ya mashine  hiyo.
Aidha alisema  mashine ilikuwa modeli ya zamani (6 slices), upatikanaji  wa vipuri  ulikuwa mgumu .Taratibu za uagizaji  na ununuzi wa vipuri  zilifanyika na matengenezo  yalikamilika mwishoni  mwa Desemba ,2012.
Kwa sasa hivi mashine  ya CT- Scan  ya MNH, inafanya kazi vizuri ,na wagonjwa  wanapatiwa  huduma.Tatizo la mrundikano wa wagonjwa  wa huduma hiyo halipo tena.