Serikali Yatahadhalishwa Mauaji ya Mkoani Mara

George Marato-Musoma

SIKU chache baada ya kutokea kwa mauji ya kinyama na kutisha katika wilaya za Butiama na Musoma mkoani Mara,Serikali imeombwa kuacha mdhaa na kuingizasiasa hivyo kusababisha kushindwa kuchukua hatua za haraka za haraka za kudhibiti ukatili huo ambao umesabisha hofu kubwa kwa wananchi.
Akizungumza na Radio One Stereo kwa njia ya simu kutoka nchini Marekani,mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono,ambaye yuko nchini humo kwa matibabu,amesema amesikitishwa na serikali kupitia Jeshi la Polisi kushindwa kuchukua hatua ambazo zitawezesha kukamatwa kwa watu wanahusika na unyama huo.
Amesema vitendo hivyo vya mauji ya kikatili,inawezekana vinahusisha watu wakubwa na wenye uwezo kifedha hivyo hatua ya Jeshi la Polisi kuendelea kukamata watu ili kujitoa katika dimbwi la lawama kutazidisha kuhimarisha zaidi mtandao huo na hivyo kutishia maisha ya wananchi wa maeneo hayo.
Pamoja na kutoa pole kwa wananchi wake kufuatia wimbi hilo la mauji hayo yanayoendelea jimboni kwake wilayani Butiama,mbunge huyo amelishauri jeshi la polisi kutumia kipimo cha vina saba DNA kwaajili ya kupambana na mtandao wa ukatili huo ambao umesababisha hofu kwa wananchi hata kushindwa kwenda mashambani kwa kuogopa kukamatwa na kuchinjwa.
Mbunge huyo wa Musoma vijijini amesema kama jeshi la polisi halina wataalam wa kufanya vipimo hivyo yuko tayari kuisaidia serikali kutafuta wataalam hao katika nchi ya Marekani na Uingereza ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na unyama huo.
Tayari watu zaidi ya watatu wameuawa kwa kuchinjwa mithili ya kuku huku wauaji wakiondoka na viungo vyao vikiwemo vichwa ambapo zaidi ya watu kumi pia wameuawa kwa mapanga kwa nia hiyo hiyo ndani ya mwezi mmoja katika wilaya ya Butiama na Musoma mauji ambayo yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina katika uchimbaji wa madini na uvuvi wa samaki.