Dodoma
SERIKALI imemsafisha aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge kwa madai kuwa hahusi na kashfa ya Rada na kutaka mwenye ushahidi apeleke na serikali itaupokea na kumfikisha kwenye vyombo vya dola.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe alimsafisha Chenge Bungeni jana wakati anahitimisha hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2011/2012 ya wizara yake.
“Kumekuwa na madai mengi kwamba Chenge anahusika na kashfa ya Rada, lakini uchunguzi uliofanywa na SFO ulibaini kwamba Chenge hakuhusika na sakata hilo kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
…Wahusika na kashfa hii ni mawakala wa BAE system, Christopher …., Jonathan na …wote raia wa Uingereza. Huwezi kwenda mahakamani bila ushahidi, hivyo kama kuna mtu, mbunge au taasisi ana ushahidi alete na Serikali itaupokea,” alisema Chikawe.
CHANZO; Jambo Leo