Serikali ‘Yaifagilia UCA-Tanzania’ Kuwanyanyua Vijana

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa UCA-Tz, Emmanuel Mushy akizungumza na vijana kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya uzinduzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa UCA-Tz, Emmanuel Mushy akizungumza na vijana kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya uzinduzi.

Baadhi ya wasanii chipukizi wa muziki na sanaa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya viongozi wa UCA-Tanzania.

Baadhi ya wasanii chipukizi wa muziki na sanaa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya viongozi wa UCA-Tanzania.

Mmoja wa wasanii wa kuchora akionesha kipaji chake cha kuchora michoro anuai kwa jamii kwenye tamasha hilo

Mmoja wa wasanii wa kuchora akionesha kipaji chake cha kuchora michoro anuai kwa jamii kwenye tamasha hilo

IMG_3968

IMG_4010

IMG_3950

IMG_3948

IMG_3913

IMG_3910

IMG_3868

 

Picha mbalimbali juu ni baadhi ya wasanii chipukizi wakionesha vipaji vyao kwenye tamasha hilo.

Baadhi ya wasanii chipukizi wakimsikiliza mgeni rasmi kabla ya kuonesha vipaji vyao.

Baadhi ya wasanii chipukizi wakimsikiliza mgeni rasmi kabla ya kuonesha vipaji vyao.

Baadhi ya wasanii chipukizi wakimsikiliza mgeni rasmi kabla ya kuonesha vipaji vyao.

 

Baadhi ya Wasanii chipukizi mbalimbali waliopata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwenye tamasha hilo.

IMG_4052

 Msanii anaoanza kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Ally Nipishe akiwaunga mkono wasanii chipukizi katika tamasha hilo.

IMG_4040

 Msanii anaoanza kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Ally Nipishe (kushoto) akiwaunga mkono wasanii chipukizi katika tamasha hilo pamoja na msanii kutoka nyumba ya vipaji THT.

IMG_4017

 

Mmoja wa wasanii chipukizi akifanya vitu vyake jukwaani.

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameipongeza Asasi ya Ukuzaji Vipaji vya Sanaa na Muziki nchini (UCA-Tanzania) kwa wasanii chipukizi. Pongezi hizo zimetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Bi. Kihimbi alisema hayo alipokuwa akizinduwa tamasha la ukuzaji Vipaji vya Sanaa na Muziki kwa vijana lililoandaliwa na asasi ya UCA-Tz kwa lengo la kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji kuonesha vipaji vyao kwa jamii kila mwaka.

“…Nimeambiwa kuwa asasi hii imesajiliwa kwa lengo la kuwashirikisha na kuwaunganisha vijana wenye vipaji vya sanaa na muziki pamoja na waliokwishafanikiwa katika kuwezesha kukuza vipaji walivyonavyo,” alisema Bi. Kihimbi akimuwakilisha Katibu Mkuu.

“Kimsingi hili ni jambo jema la kusaidiana na serikali katika kukuza vipaji na kuongeza viwango vya sanaa, ili kuwawezesha wasanii wetu kukabiliana kikamilifu katika ushindani wa soko la kimataifa,” alisema.

“…Nawashauri vijana watumie fursa kama hii kila kila zinapopatikana katika kufanikisha malengo yao kupitia fani za sanaa. Kama sote tunavyofahamu kuwa sanaa ni ajira na inanafasi kubwa ya kubadili maisha ya watu na nchi kiuchumi na kifikra ni vema watu wakaondokana na dhana potofu kuwa sanaa si kazi ya maana na ni kwa wasiohitaji kujifunza,” alisisitiza.

Aidha alitoa changamoto kwa badhi ya watu kuacha fikra finyu za kuichukulia sanaa kama si kazi kama ilivyo kazi nyingine, kwani mawazo hayo hayaitendei haki pamoja na kuzingatia umuhimi wa sanaa kwa jamii. “…Ninapata furaha kubwa kusikia kuwa tamasha hili litakuwa likifanyika kila mwaka. Ninakupongezeni sana kwa kubeba sura ya uzalendo unaolenga kuikuza, kuiendeleza na kuipa hadhi fani ya sanaa na muziki,” aliongeza.

“…Ninatambua kuwa kazi hii kubwa na nzuri mnayoifanya ni utakelezaji wa sera ya utamaduni inayosisitiza na kusimamia maadili ya Mtanzania pamoja na kuzingatia mafunzo na elimu katika fani zetu. Tunafahamu kuwa utamaduni ni mali ya jamii, hivyo ni jukumu la wananchi wenyewe kuupenda, kuuthamini na kuuendeleza utamaduni wetu kwa kutumia kazi za sanaa.”

Awali akizungumza kabla ya uzinduzi wa tamasha hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa UCA-Tz, Emmanuel Mushy aliishukuru Serikali kwa ushirikiano iliouonesha kufanikisha tamasha hilo na kutoa shukrani kwa makampuni ya Zantel, Coca Cola- Tanzania, Maezeki, LBGY Media na mtandao wa dev.kisakuzi.com kushiriki kuwasaidia vijana wasiosikika kusikika.

Zaidi ya wasanii 25 chipukizi walipata nafasi kwenye tamasha hilo ya kuonesha uwezo wao kwa jamii wakiwemo baadhi ya wasanii chipukizi wanaoanza kunufaika na kazi zao kama Menina, M Rap na Ally Nipishe.