Serikali Yaendelea Kuibana Tanesco…!

Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dk. Medadi Kalemani (wa kwanza kushoto) akitoa maagizo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya SAE Power Lines Bw. Stephen Joseph (wa kwanza kulia) anayejenga Mradi wa TEDAP eneo la Gongo la Mboto kuhakikisha umeme unaanza kuwaka katika mitambo hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba 2015 kwa kuwa kila kitu kimeshakamilika katika mradi huo na malipo yake tayari ameshamaliziwa kulipwa, (wapili kushoto) ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw. Gregory Chegere.

Na Ally Daud, Maelezo

SERIKALI imeliagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kukamilisha mradi wa kukuza miundo mbinu ya kusafirisha umeme unaosimamiwa na Kampuni ya kutengeneza vipozeo (Transformer) ya Italy (SAE) ili kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika. Agizo hilo limetolewa jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kaleman katika ziara yake ya kutembelea mradi huo katika vituo vya Mbagala, Kurasini, Gongo la Mboto na kipawa.

Amesema kuwa ni vema hadi kufikia Februari mwakani Tanesco wawe wamekamilisha mradi huo na wananchi waweze kupatiwa huduma ya umeme haraka iwezekanavyo. Aidha Dk. Kalemani aliagiza kuwa kutokana na kesi ya fidia ya wananchi wote ambao wameondolewa kwenye maeneo yao ili kupisha mradi huo ni vema wawe wamelipwa kufika Januari 2016.

Akitoa maelezo kwa Naibu Waziri huyo, Meneja Mradi wa Tanesco Mhandisi Frank Mashalo amesema kuwa kulingana na mkataba walioingia na Kampuni ya SAE mradi huo ulipaswa kukamilika kwa kipindi cha miezi 18 lakini bado haujakamilika kutokana na vikwazo mbalimbali ikiwemo sakata la fidia na kuchelewa kwa vipozeo vya umeme kufika kwenye vituo hivyo. Ameongeza kuwa jumla ya dola milioni 34.252 zinatarajiwa kutumika ili kukamilisha mradi huo ambapo kati ya hizo tayari Dola milioni 28 zimeshalipwa.