Serikali Yaahidi Kuisaidia NIDA Kufikia Malengo

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wa pili kushoto) akishikana miono na meza kuu kuonesha umoja na Baraza la Wafanyakazi la NIDA.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wa pili kushoto) akishikana miono na meza kuu kuonesha umoja na Baraza la Wafanyakazi la NIDA.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ndugu Dickson E. Maimu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ndugu Dickson E. Maimu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ndugu Dickson E. Maimu (wa pili shoto) pamoja na wafanyakazi na maofisa wa NIDA.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ndugu Dickson E. Maimu (wa pili shoto) pamoja na wafanyakazi na maofisa wa NIDA.

Picha ya pamoja na mgeni rasmi, kwa washiriki wa baraza hilo pamoja na viongozi wakuu wa NIDA.

Picha ya pamoja na mgeni rasmi, kwa washiriki wa baraza hilo pamoja na viongozi wakuu wa NIDA.


NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima leo amefungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kilichofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach ukumbi wa Kambarage, Dar-es-salaam na kuahidi serikali kuendelea kusaidia NIDA ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya Nne ya kila mtanzania kuwa amesajiliwa na kupata Kitambulisho chake.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ndugu Dickson E. Maimu, amesema mpaka sasa NIDA imepiga hatua kubwa katika zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu na ugawaji wa Vitambulisho vya Tafa.
Mpaka sasa NIDA imefanikiwa kusajili wananchi mil 6.1, ambapo kati ya hao wananchi mil 2.8 tayari wameshakamilisha hatua za usajili kwa maana ya kuchukuliwa alama za kibaiolojia kwa Zanzibar na Bara. Jumla ya Vitambulisho mil 1.7 vimezalishwa na kugawanywa kwa wananchi. NIDA tayari imekamilisha usajili wa awali Tanzania Zanzibar, mkoa wa Dar-es-salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, na Tanga
Akielezea changamoto kubwa ya sasa inayoikabili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ndugu Maimu ameeleza changamoto kubwa kuwa ni rasilimali fedha na rasilimali watu na hivyo kuzorotesha utendaji na mikakati ya kuendelea na Usajili katika mikoa ya Tanzania.
Amesema mipango ya sasa ni kuanza rasmi kwa matumizi ya Vitambulisho vya Taifa, na tayari vikao na wadau wanufaika vimeshafanyika kwa Bara na Visiwani, na muda si mrefu Vitambulisho vitaanza kutumika kama nyaraka rasmi ya utambulisho.
Akizungumza na wafanyakazi hao, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mhe. Pereira ameahidi serikali kupitia Wizara yake kuendelea kuongezea nguvu Mamlaka kufikia malengo iliyojiwekea.
Amewataka wajumbe wa Baraza hilo kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuishauri vizuri Taasisi kufikia malengo yake na kutazama mambo katika mtazamo mpana, ili kuhakikisha changamoto zinazojitokeza kutafutiwa mikakatii ya pamoja ili kila Mtanzania mwenye sifa, mgeni Mkaazi na Mkimbizi aweze kupata haki yake msingi ya kikatiba ya kusajiliwa na kupata kitambulisho chake kwa wakati na kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria zilizowekwa.
Amesema NIDA ina wajibu na dhamana kubwa katika usalama wa nchi kama zilivyo taasisi nyingine za namna hii, hivyo hawana budi kuhakikisha mradi huu unatekelezeka na wananchi ambao idadi kubwa ni masikini wana nufaika ipasavyo.
Aidha, amesisitiza wananchi na wadau mbalimbali wanaohusika katika zoezi hili, kutafuta taarifa sahihi za watu na kuelimisha zaidi Umma wa Watanzania kuhusu ufanisi utokanao na mazingira halisi ya maisha ya Mtanzania.
Amewaasa wafanyakazi wa NIDA, kila mmoja kutimiza wajibu wake kwani haki huenda na wajibu; na hivyo kuondokana na utendaji kazi kwa mazoea na kasumba ya sasa ya watumishi wa Umma kukwepa majukumu yao.
Mkutano huu utafanyika kwa siku tatu, na unatarajiwa kutoa maazimio katika kuleta ufanisi zaidi katika kuwahudumia wananchi ili waweze kunufaika na Vitambullisho vya Taifa ambavyo kwa sasa ndiyo matumaini na nyenzo kubwa ya wananchi katika Nyanja ya ulinzi na usalama, kijamii na kisiasa.