Na Jenikisa Ndile – MAELEZO
Serikali ya Tanzania na Ujerumani zimetiliana saini mikataba miwili ya misaada yenye thamani ya jumla ya Sh. Bilioni 39. 1 ambazo ni sawa na Euro milioni 17 kusaidia sekta mbalimbali nchini.
Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke ili kuleta mafanikio na maendeleo katika.
Sekta zitakazonufaika na msaada huo uliotolewa na Serikali ya Ujerumani ni pamoja na sekta ya afya, maji na maliasili. Aidha, Dk. Likwelile amemhakikishia Balozi Kochanke na ujumbe wake kuwa msaada walioipa Serikali utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta ufanisi na kuongeza nafasi za ajira na hatimaye kuchangia katika kuboresha uchumi nchini.
Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke amesema kuwa serikali ya Ujerumani itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Zaidi ya hayo, serikali hizo mbili zimesaini mkataba wenye thamani ya Euro milioni 10 ambazo ni sawa na bilioni 23 za kitanzania kuisaidia usimamizi wa hifadhi ya taifa ya Selous