Serikali ya Tanzania ya Ufaransa Zimesaini Mkataba wa sh. bilioni 223

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wa sh. Biloni 223 kwa niaba ya Serikali Tanzania ambapo makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi Ufaransa nchini Malika Berak.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano mara baada ya kusaini ambapo hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi Ufaransa nchini Malika Berak.

Na Eleuteri Mangi- MAELEZO

Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) imesaini makubaliano ya mkopo nafuu wenye thamani ya Sh. bilioni 223 za Kitanzania ambazo ni sawa Euro milioni 93 kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya maji na umeme nchini.

Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam ambapo kwa upande wa Tanzania Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua amesaini kwa niaba ya Serikali na kwa upande wa Serikali ya Ufaransa imewakilishwa na Balozi wake nchini Malika Berak na Mwakilishi wa AFD Yves Boudot.

Dkt. Mwinyimvua amesema kuwa fedha hizo kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa zimetolewa kwa ajili ya kutiasaini mikataba mitatu ili boresha upatikanaji wa huduma za jamii.

Mkataba wa kwanza unahusisha sekta ya maji ambao wenye thamani ya Euro milioni 40 utakaosaidia kuboresha huduma ya uzalishaji maji, utunzaji maji safi na salama pamoja na kuboresha huduma ya maji taka nchini katika maeneo ya mijini na vijijini.

Dkt. Mwinyimvua alisisitiza kuwa mkataba wa pili una thamani ya Euro milioni 53 kwa lengo la uboreshaji wa sekta ya umeme nchini ambapo vituo 10 vilivyo chini ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na vitanufaika na mkopo huo ili kutakarabati mtandao wa miundo mbinu ya umeme na kukabiliana na upotevu wa umeme nchini.

Vituo hivyo vitakavyokarabatiwa ni Chalinze, Mlandizi, Same, Tabora, Mbeya, Mufindi, Dodoma, Mwanza na Bukoba pamoja na Mkongo wa Taifa.

Na mkataba wa tatu unahusisha mkataba wa Tanzania na Ufaransa wa mwaka 1998 ambao ni umekuwa wa muda mrefu ili kuendana na hali ya sasa ambapo yametokea mabadiliko mengi ambayo yanapaswa kuendana na wakati.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha ushrikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Ushirikiano wa Tanzania na Ufaransa katika miradi ya maji na umeme umekuwa na tija kwa wananchi kijamii na kiuchumi tangu miaka ya 2009 ambapo Shirika la AFD lilitoa zaidi ya sh. Bilioni 628.