Serikali Lawamani kwa Kutowekeza -Mara

Na Mwandishi wa Mwana wa Afrika
MUSOMA

WANANCHI Mbalimbali mkoani Mara wameilalamikiaSerikali kwa kutowekeza katika elimu ya juu katika mkoa huu wa Kihistoria hapa nchini.

Wakiongea kwa Nyakati tofauti na mwandishi wa habari hii,wananchi hao walisema kuwa msimu huu kwasasa ni msimu wa wanafunzi kumaliza Shahada zao na shahada za juu lakini kwa Mkoa wa Mara hakuna kitu kama hicho kinachoonekana hapa.

Walisema kuwa kutokuwepo kwa vyuo vinavyotoa elimu ya Juu hapa MKoani Mara husababisha hata suala la Maendeleo linakuwa la kusuasua kutokana na eneo kubwa kutokuwa na Wasomi wa kutosha.

“Kiukweli hili ni tatizo la Serikali kwani mkoa huu hakuna chuo kinachotoa Elimu ya Juu hivyo wasomi hakuna na kutokuwepo kwa Wasomi ni tabu maana Jamii itabaki katika mawazo Mgando” alisema Mzee Magesa John mtumishi mstaafu.

Mzee Magesa alisema kuwa Mikoa mingi Tanzania yenye vyuo vinavyotoa Elimu ya juu imekuwa na Mwamko mkubwa wa Jamii katika suala la Maendeleo tofauti na hapa Mara kwani hakuna chuo chochote ambacho kingeweza kuleta hata changamoto kwa Wazazi kuona umuhimu wa Elimu kwa vijana wao.

Akimuunga kuhusu Suala hilo Mwalimu Emanuel Ghati naye alisema kuwa ni kweli kukosekana kwa Chuo kinachotoa shahada katika mkoa huu ni kuendelea kuwatenga wana Mara katika suala la Elimu,Mwali Ghati alisema kuwa ingekuwa rahisi kwa watu kujiendeleza wanapotoka Kazini kuliko ilivo hivi sasa ambapo watu wengi wakipangwa Kikazi Mara hawapendi kufanya kazi mkoa kutokana na kutokuwa na mambo mengi.

“Hii ni kweli maana kuja kufanya kazi huku kunapelekea kupoteza fursa nyingi hasa suala la elimu kwani Mkoa kama Mwanza umeendelea kwa sababu una Vyuo ambavyo kwanza vimesababisha Muingiliano kuwa mkubwa lakini pia vimesaidia Mwamko katika Jamii” alisema Mwl Ghati.

Naye Juma Jambo akitolea mfano Chuo kikuu cha Dodoma kilivyojengwa haraka na kuanza kutoa huduma alihoji inakuwa Serikali kupitia wizara ya Maendeleo ya Jamii,jinsia na watoto inashindwa kupandisha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kitoe kiwango cha Digree.

Alisema chuo cha Kikuu cha Arusha kilichopo si msaada wa wana Mara kwani hicho ni chuo ambacho kipo katika kujenga faida na si kuwasaidia Watanzania,hivyo Basi Jambo aliongeza kuwa anadhani ni muda muafaka kwa serikali kuona umuhimu wa kupandisha chuo cha Buhare kutoa kiwango cha Digree.

“Mbona chuo cha Dodoma kilijengwa kwa muda mfupi na kuanza kazi iweje sisi Mara tusahaulike na kwanini Serikali isikipandishe chuo cha Buhare kutoa digree ? alihoji bwa Juma Jambo mkazi wa Makoko mjini hapa.