Woinde shizza, Arusha
SERIKALI ya awamu ya tano imesema kuwa itaendeleza jitihada za
kutunza na kulinda urithi wa dunia ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi
wanaoishi maeneo ya uhifadhi ili watanzania wote waweze kunufaikana
rasilimali za nchi .
Hayo yalisemwa na waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati akifungua mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa afrika kama nyenzo ya maendeleo endelevu unaoendelea mjini hapa.
Majaliwa alisema kuwa rasilimali zilizopo ni za watanzania na ili
kuhakikisha kuwa wananufaika nazoserikali itahakikisha inatunza na
kulinda uhifadhi ili yawe endelevu na kuweza kusaidia vizazi vijavyo.
Alidai kuwa Tanzania ni moja ya tajiri wenye urithi na hivyo ili
kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika haswa waishio maeneo ya uhifadhi
serikali itatoa elimu ya kutosha ili waepuke kuchangia uharibifu
unaotokea kwenye hifadhi za taifa na hivyo kusababisha kuongezeka kwa uchumi wa taifa na hata wananchi wenyewe.
“Rasilimali hizi ni zetu na hivyo hata wanaoishi maeneo ya hifadhi
watusaidie kwa wale wanaoingilia na kuharibu kwani hata hizo mali
asili zinatusaidia sote na hata tumewekea mikakati ya kutunza maeneo
hayo ili yawe endelevu’alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni katibu mkuu wizara ya mali asili na utalii meja jenerali Gaudence Milanzi Alisema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo yanatishia na kuadhiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia katika Afrika.
Aidha mkutano huo utapendekeza suluisho kwa kupitia upya shughuli
zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.
Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku inayotokea kwenye maeneo urithi wa dunia kutokana na makundi ya kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.
Aliongeza kuwa pia mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO ya
mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa uridhi wa dunia.
“Mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia uatakuwa na manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali
pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageniwatakao
uthudhuria mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na kujenga mataji wa kijamii”alisema Malinzi
Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro