Serikali Kuendelea Kuwekeza Kwenye Utafiti na Ubunifu

Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati akifungua Kongamano la nne la Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi.

Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati akifungua Kongamano la nne la Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayojishughulisha na Utafiti wa Sayansi ya Jamii (REPOA), Profesa Samuel Wangwe akitoa hutuba  mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda akizungumza katika uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa meza kuu na viongozi wengine. Kulia ni Waziri wa Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbawara na Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Kanali mstaafu Joseph Simbakalia.
Wadau wa masuala ya sayansi wakiwa kwenye kongamano hilo.

Wadau wa masuala ya sayansi wakiwa kwenye kongamano hilo.

Wanahabari wakiwa kwenye kongamano hilo la kimataifa.
Kongamano likiendelea

Na Dotto Mwaibale

RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali itaendelea kuwekeza kwenye watafiti na wabunifu ili kuliletea taifa maendeleo na kuleta mapinduzi ya viwanda ili kufikia uchumi wa kati ulioimara ifikapo mwaka 2025. Pia imeelezwa kuwa utafiti unanafasi kubwa sana katika kulinufaisha taifa kwasababu kama hakuna ubunifi na utafiti hakuna sekta itakayoendelea nchini.

Rais  Jakaya Kikwete ameyasema hayo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akifungua kongamano la nne la watafiti na wabunifu wa sayansi na teknolojia. Kikwete alisema hakuna nchi yoyote duniani ile iliyoendelea bila kuwa na watafiti pamoja na wabunifu katika masuala ya sayansi na teknolojia kuiwekeza kwe watafiti kunalipa.

”Tunapozungumza mapinduzi ya viwanda ambayo yanatupeleka kwenye uchumi wa viwanda ulioimara mwaka 2025 ni lazima tufikirie kuwa na wataalamu na wanataaluma ambao ni watafiti na wabunifu ili kujenga miondombinu ya viwanda”alisema.

Alifafanua kuwa viwanda ambavyo vinaanzishwa na kuendelezwa katika karine hii ni viwanda vya kisasa ambavyo vinahitaji teknolojia na ubunifu wa kiwango cha juu na kama hakuna wataalamu itakuwa ni kazi bure.

Kikwete alisema anashukuru kufanya maamuzi mazito katika kipindi chake cha uongozi kwa kuhahakikisha anaendeleza sekta ya sayansi na teknolojia kwa kuongeza bajeti ya fedha katika kitengo cha utafiti.

”Naamini Rais atakayenibadili ataendeleza juhudi hizi na kuweza kujenga nchi yenye uchumi imara kwa kuhakikisha watafiti wanaendelezwa kwajili ya mapinduzi ya viwanda nchini kwasababu hatuendelea kwa kununua kwa wenzetu lazima na sisi tutengeneze na tuuze nje ili kuingiza mapato,”alisema.

Alifafanua kuwa kwa kipindi cha miaka ya 2010 hadi 2005 kitengo cha utafiti kilikuwa kinapangiwa bajeti ya shilingi milioni 35 ambazo zilikuwa hazikidhi mahitaji.

”Nilivyona hivyo niliangiza waziri husika kupandisha kiwango hicho ili kuwapa watafiti nafasi ya kufanya kazi zao kwa umakini na sasa kitengo kinapewa bilioni 10,”alisema.

Kikwete alisema matokeo ya jitihada za kuwaendeleza watafiki zimeshaanza kuonekana huku akimtolea mfano mtafiki aliye gundua dawa ya ugonjwa wa kuku wa mdondo kwamba yeye peke yake ameweza kuliingizia taifa sh. bilioni 186.

”Mbali na hilo alisema hadi sasa watu wapatao 517 wamenufaika kwa kufadhiriwa na kusoma masomo ya sayansi ya utafiti kwa ngazi ya shahada ya udhamivu watu 344 na phd watu 175,” alisema.