Serikali Kuboresha Utendaji Kazi wa Utumishi wa Umma

Baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi  kupitia njia ya video kwa makatibu tawala wa mikoa na wasaidizi wao, wakurugenzi wa mamlaka za serikali  za mitaa na wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu katika mamlaka za serikali za mitaa  kwenye  mikoa ya Dares Salaam, Kagera, Tanga,Tabora,Manyara, Morogoro, Rukwa na Katavi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo jijini Dares Salaam.

Baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi kupitia njia ya video kwa makatibu tawala wa mikoa na wasaidizi wao, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu katika mamlaka za serikali za mitaa kwenye mikoa ya Dares Salaam, Kagera, Tanga,Tabora,Manyara, Morogoro, Rukwa na Katavi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo jijini Dares Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Mafunzo kwa Mtandao(TaGLA), Charles Senkondo akifafanua jambo kuhusu matumizi ya njia ya video leo leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo jijini Dares Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Mafunzo kwa Mtandao(TaGLA), Charles Senkondo akifafanua jambo kuhusu matumizi ya njia ya video leo leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo jijini Dares Salaam


Na Magreth Kinabo na Anna Nkinda
Serikali imefanikiwa kuboresha utendaji kazi wa utumishi wa umma kwa kuendesha mikutano kupitia njia ya video(TEHAMA) katika taasisi zake,wizara idara ili kuongeza kwa ufanisi na tija kwa gharama nafuu kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwa muda mfupi.

Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uendeshaji wa kikao kazi kupitia njia ya video kwa makatibu tawala wa mikoa na wasaidizi wao, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu katika mamlaka za serikali za mitaa kwenye mikoa ya Dares Salaam, Kagera, Tanga,Tabora,Manyara, Morogoro, Rukwa na Katavi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo jijini Dares Salaam.

“Serikali imebuni sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao katika kutekeleza majukumu yetu kwa kulenga tija na ufanisi. Leo tunazungumzia mpango wa Matokeo Mkubwa Sasa (BRN) ili tupate matokeo ya BRN kwa ufanisi na kwa wakati hatuna budi kutumia TEHAMA,” alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo.

Mkwizu alisema mkutano huo ni wa awamu ya kwanza kufanyika kwa kupitia njia hiyo, hivyo vikao vitatu vimefanyika, kikao cha kwanza kufanyika kilifanyika Septemba 15,mwaka huu ambao ulihusisha watendaji hao kwenye mikoa ya Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Dodoma , Ruvuma Kigoma,Lindi na Geita.

Aliongeza kwamba mkutano wa awamu ya pili ulifanyika Septemba 17, mwaka huu ambapo ulihusisha watendaji hao kwenye mikoa ya Arusha, Singida,Pwani,Iringa, Mara,Mtwara, Shinyanga, Njombe na Simiyu.

Alizitaja mada zilizojadiliwa katika mikutano hiyo kuwa ni Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 na kanuni zake, wajibu wa waajiri katika ufuatiliaji na uzingatiaji wa maadili katika utumishi wa umma , ukaguzi wa rasilimali watu katika utumishi wa umma, ambalo ni jukumu la msingi la Tume ya Utumishi wa Umma,ambao wanakagua mifumo yamenejimmenti rasilimali watu ya utumishi wa umma na kuona inatekelezwa vipi na tathimini ya kazi katika utumishi wa umma ili kulinganisha kazi mbalimbali na hatimaye kuja na mapendekezo kazi mbalimbali watu walipwe vipi kulingana na unyeti, madaraka ili zinazofanana zilipwe sawa na zisizofanana zilipwe tofauti.

Alisema awamu ya pili ya uendeshaji wa mikutano kwa kutumia njia hiyo itafanyika Novemba mwaka huu.
Mkwizu alifafanua kwamba tayari Serikali imeshaweka mwongozo katika taasisi zake na mamlaka za Serikali ili ziweze kufanya mikutano au kikao kazi kwa njia video. Hivyo mikoa yote imeshafungiwa vifaa maalum kwa ajili ya matumizi hayo isipokuwa mikoa mipya ambayo ambayo hujiunga na mikoa mama.

Kwa upande wake Mkurungezi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo wa Serikali Mtandao(TaGLA), Charles Senkondo alisema ulianzishwa mwaka 2011 ili kuongeza kasi ya uboreshaji wa huduma.

Alisema mfumo huo umewezesha madaktari bingwa wa hapa nchini kuweza kutibu wagonjwa kwa kuwasiliana na madaktari wenzao mabingwa kutoka nje ya nchi, watu kufanya usaili na kupata kazi za kimataifa na mahakama kuendesha kesi kwa kuwasiliana na mashahidi walioko nje ya nchi.

Alizitaja changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na baadhi ya watu kuwa na fikra potofu katika matumizi ya TEHAMA, wengine wanafikiri ni kitu kigumu na kuwa na woga wa kutumia lakini kutokana na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wadau mbalimbali wameendesha mikutano mingi na wanao uwezo wa kutoa ushauri na mwongozo inayosaidia kuendesha mikutano kupitia njia hiyo ili iweze kufanyika vizuri.

“Watanzania wafahamu kwamba wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao imeanzishwa na Serikali kwa ajili yao, hivyo ninatoa wito waweze kuitumia na kupeleka taarifa kwa urahisi ambazo zinawafikia watu wengi kwa wakati mmoja na sisi tuko tayari kutoa ushauri ili mikutano kufanyika ipasavyo”, alisema Senkondo.