Serikali Kubeba Gharama za Msiba wa Brigedia Hashim Mbita

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) alipomtembelea Brigedia Hashim Mbita.

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) alipomtembelea Brigedia Hashim Mbita akiwa hospitalini enzi za uhai wake.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mtumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ) na Chama cha TANU na Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika kwa miaka mingi, Brigedia Hashim Mbita.

Mzee Mbita ambaye amekuwa anauguza afya yake kwa muda sasa amefariki asubuhi ya leo, Jumapili, Aprili 26, 2015 mjini Dar Es Salaam. Kufuatia taarifa za msiba huo, Rais Kikwete ameelekeza Serikali na Jeshi kushirikiana na familia kusimamia msiba huo na kuandaa mazishi ya Mzee huyo.