MAELFU ya wapenda burudani mjini Mbeya walijitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Sokoine jijini humo kushiriki katika Tamasha la Serengeti Fiesta. Tofauti na ilivyotarajiwa, idadi kubwa ya wananchi wa mkoa huo walijitokeza na kuufunika Uwanja wa Sokoine kwa shangwe mwanzo hadi mwisho.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager ambayo ndio bia inayodhamini tamasha hili kubwa, Allan Chonjo alisema ”Mpaka sasa tumepata wawakilishi sita kutoka Mtwara na Linda waliopata nafasi ya wageni maalum (VIP) ambao ni Jovin Manzi, Mary Joseph, Baraka Shaban, Issa Shabani, Benard Boniface”.
”Washindi wote kutika mikoani watakaa jukwaa la watu maalumu ambapo wataweza kushuhudia burudani kwa karibu zaidi na watapata nafasi ya kupiga picha na wasanii wakubwa, hivyo tunawaomba wakazi wa Mtwara waendelee kunywa bia ya Serengeti ili waweze kujishindia bia za bure na hatimaye kushinda nafasi hiyo ya kuja Dar Es Salaam kwa ajili ya Fiesta ya mwisho”. Wateja wanatakiwa kuangalia chini ya kizibo na kuona kama wajishindia bia za bure, kwani kuna bia zaidi ya laki mbilli nchi nzima, aliongeza Chonjo.
Mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo, Simon Simalenga alikiri kushangazwa na umati mkubwa uliojitokeza ukilinganisha na mikoa mingine ambayo tayari Fiesta imeshapita.
“Watu wamekuwa wengi kinyume na matarajio ila tunafurahi wameburudika na burudani iliyodondoshwa”
Katika tamasha hilo msanii Quick rocka mkali wa kurap ambaye pia ni mwenyeji wa mji huo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwachezesha maelfu ya watu waliokuwapo uwanjani hapo kupitia ngoma zake kali.
Pamoja na mwenyeji huyo wasanii kibao walifanya vizuri akiwamo Ney wa Mitego, Madee, Juma Nature, Shilole, Walter Chilambo, Stamina, Young Killer na Godzilla. Shangwe ziliibuka upya Ney wa mitego alipopanda stejini na kuimba wimbo ulioimbwa na mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Wengine ni Afande Sele, Ommy Dimpoz, Rich Mavoko, Chege, Temba, Kassim Mganga, Joh Makini na Nick wa Pili. Orodha hiyo hiyo inatarajiwa kutoa burudani siku ya leo kwa wakazi wa Mji wa Iringa.