Serengeti Dance la Fiesta 2012 Moshi

Mmoja wa majaji wa shindano la   Serengeti Dance la Fiesta 2012 lililofanyika kwenye Club ya Mawingu jioni ya leo, jijini Arusha, Hamis Mandi a.k.a B Dozen kutoka kipindi cha XXL kinachorushwa na redio ya Clouds FM, akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa kundi shindi la shindano hilo liitwalo Contagious Crew

Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya SBL, wakimkabidhi mmoja wa wacheza shoo wa kundi la News Contagious Crew kreti la bia ya Serebgeti, mara baada ya kuibuka washindi wa shindano la    Serengeti Dance la Fiesta 2012, washindi wa pili walikuwa ni kundi la New Kings ambao wao walijinyakulia kreti la bia.
Mwendesha shindano hilo pichani kati, Nikson akisoma majina ya makundi mawili yaliyoingia fainali na hatimae kulipata kundi moja mahiri kabisa na  kundi la Contigious Crew limeibuka mshindi na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja taslim na kreti moja ya bia ya Serengeti, ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2012.