Serengeti Breweries yazindua kampeni za tutashinda

Na Joachim Mushi

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji chake cha Serengeti imezindua kampeni ya wananchi kuiunga mkono Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ya Tanzania ili kuwapa nguvu wachwzaji kuweza kufanya vizuri kwenye mashindano yanayokuja.

Akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, Teddy Mapunda amesema kampuni ya SBL kama mdhamini mkuu wa timu ya Taifa itaendelea kuunga mkono timu hiyo kuelekea mafanikio.

Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi katikati akizindua kampeni za kuhamasisha ushindi kwa timu ya taifa ya Tanzania zilizoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL).


Amesema SBL kwa sasa inaelekeza nguvu zake za ufadhili kwa timu ya taifa katika mchezo wake wa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad inayotarajiwa kufanyika Novemba 11, 2011 jijini N’Djamena. Aidha Bi. Mapunda amesema SBL itazunguka katika baadhi ya mikoa na kuwahamasisha wananchi kuiunga mkono timu ya taifa kwa kauli inayosema ‘Tupo pamoja na Tutashinda’ kauli ambayo unaonesha umoja na ushirikiano.

Akizungumza kabla ya kuzindua kampeni hizo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malizi aliishukuru SBL kwa kukubali kuidhamini timu ya taifa na moyo inaouonesha wa kuinua mpira na michezo mingine nchini. Uzinduzi huo pia uliudhuriwa na Raisa wa TFF, Kocha Mkuu wa Taifa Jan Poulsen na viongozi wengine waandamizi wa TFF na BMT.

Tayari juzi Kocha Mkuu Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 22 ambao wanaunda kikosi cha timu ya taifa Chad itakayochezwa Novemba 11 jijini N’Djamena.