
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Epraimu Mafuru akipiga danadana kwenye hafla ya kuwapongeza washindi wawili wa Fainali za Guinness Football Challenge. Wengine ni washirikia wa mashindano hayo kutoka tanzania katika picha ya pamoja.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Guinness Football Challenge katika picha ya pamoja huku wakionesha manjonjo ya kucheza na mpira


Mmoja wa viongozi wa bia ya Guinness akionesha umahiri wa kuchezea mpira katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel JB Belmont.

Wageni waalikwa pia walijishindia zawadi mbalimbali kutoka SBL kupitia kinywaji chake cha Guinness baada ya kushinda michezo anuai iliyokuwa ikiendeshwa ndani ya hafla hiyo.
