Serengeti Breweries Wazindua Tupo Pamoja Katika Shangwe za Mafanikio

Viongozi wa SBL, kutoka kushoto ni Iman Rwinga, Ephraim Mafuru na Allan Chonjo wakizungumza na wanahabari na wageni wa alikwa juu ya uzinduzi wa kampeni za Tupo Pamoja Katika Shangwe za Mafanikio.

Mkurugenzi wa Masoko SBL, Ephraim Mafuru(wa pili kushoto) akifafanua uzinduzi wa kampeni za Tupo Pamoja Katika Shangwe za Mafanikio.

Meneja wa Bia ya Serengeti, Allan Chonjo

Na dev.kisakuzi.com

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) leo imezindua kampeni mpya za matangazo kuitangaza bia yake maarufu ya Serengeti inayopendwa na idadi kubwa ya watu. Kampeni hizo maalumu ambazo zitajulikana kama Tupo Pamoja Katika Shangwe za Mafanikio.

Akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hizo jijini Dar es Salaam ndani ya JB Belmont Hotel, Mkurugenzi wa Masoko SBL, Ephraim Mafuru amesema kampeni hizo ni maalumu kwa ajili ya kuwashukuru Watanzania ambao wamekuwa pamoja kiushirikiano katika mafanikio ya kinywaji hicho.

Alisema Watanzania wanahitaji kuthaminiwa hivyo wameona kwa kuthamini mchango wao kuna kila sababu za kusherehekea katika mafanikio. “Kampuni ya Bia ya Serengeti inatambua mchango wa kila Mtanzania katika mafanikio yake…ndiyo maana imezindua kampeni hii ya tupo pamoja katika shangwe za mafanikio,” alisema Mafuru.

Naye Meneja wa Bia ya Serengeti, Allan Chonjo akizungumza katika hafla hiyo alisema kampeni hizo zinazoanzia Mkoa wa Dar es Salaam kwa maonesho mbalimbali na burudani zitakuwa zikiendeshwa baa mbalimbali huku zikiambatana na wateja wa kinywaji hicho kujishindia zawadi anuai.

Alisema kampeni hizo zitakazoambatana na matangazo kwenye vyombo vya habari, barabarani pia zitasambazwa katika mikoa anuai ya Tanzania, huku wapenzi wa SBL kujishindia pia zawadi mbalimbali.