Na Joachim Mushi
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) mwaka huu imetenga zaidi ya sh. milioni 300 kwa ajili ya kuboresha huduma za maji nchini Tanzania maeneo mbalimbali. Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda amesema milioni 100 za kitanzania zimeelekezwa kwenye sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo mwaka huu inafanyika mkoani Iringa.
Mapunda alisema fedha hizo zitatumika kuandaa vipeperushi, vijarida; huku zaidi ya sh. milioni 200 zikilenga kwenye miradi ya maji safi na salama katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Iringa yenyewe.
“Tunasisitiza kuhusu swala la kuongezeka kwa changamoto za tatizo la maji ulimwenguni, katika utendaji kazi wetu ndani ya kampuni na hata kwenye jamii inayotuzunguka. Kama kampuni, Serengeti (SBL), inafanya kazi kupunguza matumizi ya maji katika vifaa vya uzalishaji na mfululizo wa utoaji wa bidhaa zetu.
Hii inahusisha uboreshaji madhubuti wa maji katika mitambo yetu, kuhakikisha kuwa matumizi ya maji katika maeneo yetu yanazingatiwa, na kupunguza majitaka (na nguvu ya maji hayo katika uchafuzi wa mazingira) kutoka kwenye mitambo yetu,” alisema Mapunda.
Aidha alisema SBL imekusudia kuongeza njia za upatikanaji wa maji kwenye jamii zinazotuzunguka na usimamizi wa vyanzo vya maji. Kama kampuni inayowajibika, kufanya kazi na wengine kuendeleza lengo la Umoja wa Mataifa (UN) la Malengo ya Milenia ya Maendeleo kwa ajili ya maji na usafi wa mazingira na kupitia juhudi za pamoja na wafanyakazi wetu, watumiaji, wateja, wagawaji, mashirika yasio ya kiserikali, serikali, na biashara nyingine tunafanya kazi kwa pamoja ili kuhamasisha na kutoa malengo yatakaotoa suluhisho la muda mrefu la kutatua shida ya maji katika masoko yetu.
“Programu hii ya Water of Life (WOL), imekusudia kutoa upatikanaji wa huduma ya maji safi, inaimarisha kazi tunazofanya katika utendaji wetu wa kazi. Tunatumia ujuzi, watu wanaotuzunguka washirika na wadau wetu kuhakikisha kuwa maji safi yanapatikana hasa pale yahahitajika. Kwa Jamii, majumbani na kwa watu binafsi,” alisema Mkurugenzi huyo.
“WATER of Life” (WOL), ni mpango maalum unaodhamiria kuwezesha upatikanaji wa maji safi ya kunywa na udhibiti wa usafi kwa watu wapatao milioni moja barani Afrika. Maji yamepewa kipaumbele katika biashara yetu kimataifa. Kampuni ya Bia ya Serengeti imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa maji safi na salama pamoja na usafi wa mazingira ni jambo linalotiliwa mkazo.
Wiki ya maji ambayo itaanza tarehe 16 Machi itaadhimishwa siku ya Machi 22 mwaka huu, ni jukwaa muhimu sana kutangaza na kuweka msisitizo wa umuhimu wa utunzaj wa maji na vyanzo vyake. Kwa kuiheshimu kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni “Maji kwa usalama wa Chakula”, ni dhahiri kuwa maji yanachukua nafasi kubwa sana na hasa katika ulizalishaji wa chakula na kilimo kwa ujumla.
Tatizo la maji limekuwa likiathiri kila bara duniani na zaidi ya asilimia 40 ya watu. Hadi kufikia mwaka 2025, watu bilioni 1.8 watakuwa wanaishi katika nchi ama mikoa ambayo haina maji safi kabisa, na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani inawezekana wanaishi katika hali ngumu ya upatikanaji wa maji. Kukosekana kwa maji kunawakosesha wakulima kuzalisha mazao ya kutosha kwa chakula na hata kujikimu kimaisha.
Kampuni ya bia ya Serengeti mwaka huu imetenga zaidi ya shilingi milioni mia tatu za kitanzania. Milioni mia moja za kitanzania zikilenga sherehe za maadhimisho mkoani Iringa kwa kudhamini vipeperushi, vijarida na zaidi ya shilingi milioni mia mbili zikilenga kwenye miradi salama ya maji na usafi katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dar Es Salaam na Iringa.
Tunasisitiza kuhusu swala la kuongezeka kwa changamoto za tatizo la maji ulimwenguni, katika utendaji kazi wetu ndani ya kampuni na hata kwenye jamii inayotuzunguka.
Kama kampuni, Serengeti (SBL), inafanya kazi kupunguza matumizi ya maji katika vifaa vya uzalishaji na mfululizo wa utoaji wa bidhaa zetu. Hii inahusisha uboreshaji madhubuti wa maji katika mitambo yetu, kuhakikisha kuwa matumizi ya maji katika maeneo yetu yanazingatiwa, na kupunguza majitaka (na nguvu ya maji hayo katika uchafuzi wa mazingira) kutoka kwenye mitambo yetu.
Pia tumekusudia kuongeza njia za upatikanaji wa maji kwenye jamii zinazotuzunguka na usimamizi wa vyanzo vya maji. Kama kampuni inayowajibika, kufanya kazi na wengine kuendeleza lengo la Umoja wa Mataifa (UN) la Malengo ya Milenia ya Maendeleo kwa ajili ya maji na usafi wa mazingira na kupitia juhudi za pamoja na wafanyakazi wetu, watumiaji, wateja, wagawaji, mashirika yasio ya kiserikali, serikali, na biashara nyingine tunafanya kazi kwa pamoja ili kuhamasisha na kutoa malengo yatakaotoa suluhisho la muda mrefu la kutatua shida ya maji katika masoko yetu.
Programu hii ya Water of Life (WOL), imekusudia kutoa upatikanaji wa huduma ya maji safi, inaimarisha kazi tunazofanya katika utendaji wetu wa kazi. Tunatumia ujuzi, watu wanaotuzunguka washirika na wadau wetu kuhakikisha kuwa maji safi yanapatikana hasa pale yahahitajika. Kwa Jamii, majumbani na kwa watu binafsi.
Biashara yetu imekuwa ikijihusisha na miradi mbali mbali ya maji safi na mazingira kama ‘Mkuranga water project’ na moja nyingine ambayo ilikuwa ni mradi ambao ulishirikisha makampuni na mashirika yasio ya kiserikali ni mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika hospitali ya Amana. Kampuni ya Bia ya Serengeti na EABL foundation iliwekeza kiashi shilingi milioni 384.6 za kitanzania katika mradi wa Mkuranga na zaidi ya watu 250,000 wamefaidika.
Tunatambua kwamba maji safi ni muhimu kwa maendeleo na kwa kuchangia kuboresha afya ya jamii na kiwango cha elimu na pia kupunguza umaskini. Mradi wa ‘Water Of Life (WOL) ulizinduliwa na Diageo mwezi Juni mwaka 2006 kwa lengo la kutoa maji safi ya kunywa kwa walengwa. Diageo ilizindua mradi huu katika nchi 14 nyingi zikiwa ni nchi za Afrika, kwa kusadia miradi mbali mbali ikiwemo ya uchimbaji wa visima, visima vya mkono, uvunaji wa mvua, na mbinu za kuchuja maji
Uwekezaji wetu katika jamii utaendelea kwa kusaidia na kukamilisha kazi yetu katika utendaji wetu, ili kupunguza athari za usambazaji wa maji taka na kuboresha upatikanaji wa maji safi ya kunywa katika mikoa tunayofanya shughuli zetu.
Kuhusu Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kampuni ya Bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya EABL/Diageo. Diageo ni kampuni inayoongoza duniani kwa biashara ya vinywaji ikiwa na bidhaa nyingi za pombe kali na bia. Diageo ni kampuni iliyoenea duniani, ikifanya biashara zake katika nchi 180. Kampuni hii imeorodheshwa katika soko la hisa la New York, nchini Marekani (DEO) na Soko la Hisa la Uingereza (DGE). Kampuni ya bia ya Serengeti inazalisha na kuuza bidhaa mbali mbali za bia hapa nchini ikiwa ni pamoja na Serengeti Premium Laga, Tusker, Tusker Malt , Senator, Plisner, The Kick na Uhuru Peak.
Kampuni ya Bia ya Serengeti ni msambaji pekee Tanzania wa bidhaa za Diageo zinazoongoza duniani kama Johnnie Walker Scotch Whisky, Smirnoff vodka, Vat 69, Captain Morgan, Baileys na Gilbeys gin.
Ikiwa ni moja ya muendelezo wa majukumu ya kuhudumia jamii inayotuzunguka,kustawisha maisha na kuchangia malengo ya Maendeleo la Milenia la Umoja wa Mataifa (UN Millennium Development Goal 7), Diageo Afrika imeunda mpango wa WATER OF LIFE(WOL) ili kusaidia miradi inayotoa hud)uma ya upatikanaji wa maji safi na kutoa kipaumbele katika utunzaji wa mazingira.
Hadi leo, Diageo imechangia miradi tofauti ya maji zaidi ya 100 na miradi ya udhibiti wa fya, ambapo imewanufaisha zaidi ya watu milioni 4 katika nchi 15 tofauti barani Afrika. Diageo inafanya kazi na mashirika ya kimataifa yasio ya kiserikali na pia mashirika kwenye nchi husika ili kutoa maji safi na udhibiti wa afya na kupitia njia tofauti za teknologia ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa visima vya kisasa, vichuja maji, uvunaji wa mvua na usimamizi wa usambazaji wa maji taka.