TIMU ya taifa ya Vijana ya umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys imeibuka na ushindi baada ya kuifunga Misri Mapharao mabao 2-1, katika mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu kujiandaa na michuano ya kufuzu fainali ya vijana ya mataifa ya Afrika.
Mechi hiyo iliokuwa ikichezeshwa na mwamuzi wa mwenye beji ya FIFA Israel Nkongo Serengeti Boys ilianza kupata bao dakika ya 15,kupitia mchezaji Benedicto aliyeachia shuti kali baada ya kuwatoka mabeki na wa timu hiyo na mpira kutinga wavuni.
Zikiendelea kushambuliana kwa kasi timu hizo huku Serengeti Boys ikimiliki mpira kwa asilimia 51, wakati Misri walimiliki kwa asilimia 49 hadi timu hizo zinakwenda mapunziko Serengeti Boys ilikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana huku Misri ikionyesha kutafuta bao la kusawazisha kutokana na wachezaji wake kucheza kwa kasi, iliowafanya mabeki wa Serengeti kujichanganya na mshambuliaji Diah Waheed kupachika bao la kusawazisha dakika 85.
Bao hilo liliamsha mashambulizi kwa Serengeti boys,ambao walikosa bao la pili dakika chache baada ya lile la Misri,lakini hawakukata tamaa kuendelea kutafuta pointi tatu wakiwa katika uwanja wa nyumbani.
Iliwachukua dakika ya 90, Serengeti kusawazisha bao lililofungwa na Ally Husein dakika ya 90 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18, lililomwacha kipa wa Mafarao pembeni na kutinga wavuni. Serengeti Boys watarudiana Jumanne hapa Dar es Salaam.
Chanzo: bin zubeiry.co.tz