Sepp Blatter Kutinda Mahakamani Kukata Rufaa

sepp-blatter-at-2014-fifa-congress-data

Mwanasheria wa aliyekuwa Rais wa shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp Blatter anatarajiwa kuwasilisha rufaa yake kupinga kufungiwa miaka minane kujishughulisha na masuala ya soka.

Hata hivyo kamati ya nidhamu ya FIFA imewasilisha sababu za kuchukuliwa kwa hatua za nidhamu dhidi ya viongozi hao waandamizi wa zamani wa soka Blatter na mwenzake, Michel Platini.
Mwezi Disemba aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini walifungia kwa kipindi cha miaka minane baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja kanuni na sharia za FIFA.

Kwa upande wake pia mwanasheria wa Platini anasema kuwa anatarajia kukata rufaa kwa kupinga maamuzi ya FIFA.

Wiki iliyopita Michel Platini alisema hatawania urais wa Fifa mwezi ujao
Platini, pamoja na rais wa Fifa Sepp Blatter, kwa kupigwa marufuku kutojihusisha na shughuli za soka kwa miaka minane na shirikisho hilo linalosimamia soka duniani.

FBL-FRA-EURO2016-DRAW

Wawili hao walipatikana na makosa ya ulaji rushwa kuhusiana na malipo ya £1.3m ($2m) yaliyopewa Platini mwaka 2011.
Wamekata rufaa dhidi ya marufuku hizo, lakini Platini anasema hali kwamba uchaguzi unafanyika tarehe 26 Februari ina maana kwamba hawezi akawania urais wa Fifa.”

Wagombea wa urais Fifa
• Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa – 50, Bahrain
• Tokyo Sexwale – 62, Afrika Kusini
• Prince Ali bin al-Hussein – 40, Jordan
• Gianni Infantino – 45, Uswizi
• Jerome Champagne – 57, Ufaransa