Sense Fundi Aongoza Semina Walimu Ngazi za Juu wa Karate USA

Dojo in Mesquite, TX. October 13th, 2013 218

Dojo in Mesquite, TX. October 13th, 2013 218

SENSEI Rumadha Fundi Mtanzania mtaalamu wa mchezo wa karate mwenye mkanda mweusi na dan 3, Oktoba 12 na 13, 2013 aliongoza semina ya mazoezi ya semina ya kata za karate za mtindo wa Goju Ryu huko Texas, Marekeni.

Semina hiyo iliudhuriwa na wataalamu na walimu mbalimbali wa Karate. Sensei Rumadha Fundi ambaye pia ni mwalimu wa Yoga ni mmoja ya wataalamu wachache sana wa kiafrika
wenye uwezo wa juu na kukubalika kimataifa, mtaalamu huyu mtanzania alipata mafunzo yake ya juu kule Okinawa, Japani.

Pia alisomea mambo ya Yoga nchini India. Sensei Rumadha Fundi pia ana shahada ya tiba,
utibabu wa mapafu na moyo.Watanzania wana kila sababu ya kujivunia mtoto wao Sensei Rumadha Fundi kutoka Uswahilini hadi ughaibuni.
 
Sensei Rumadha Fundi, Mtaalamu wa Karate mwenye dan tatu au (Sandan), katika mazoezi ya Kata ya ngazi za juu za mtindo wa Goju Ryu inaitwa “TENSHO”, ambayo hii ndio ilikuwa semina ya kuweza kumudu (kupiga msasa) kata za ngazi ya juu ya Okinawa Goju ryu Karate-Do.

Pia semina hiyo ilihusisha katas nyingine kama vile : Geki sa dai ichi; Geki sai da ni; Saifa;Shison chin; Sanseru; Sepai; Kururunfa, Tensho, na Sanchin. Katika picha, Sensei Rumadha na wenzie katika zoezi la kata ya “Tensho” jana octoba 12, 2013 huko Mesquite, Texas.