Na Augustine Mgendi, Musoma
SENSA ya Watu na Makazi mkoani Mara inaendelea vizuri licha ya kuwepo kwa kasoro ndogo tangu kuanza kwa shughuli hiyo Jumamosi ya Agosti 25 chini nzima.
Akizungumzia mwenendo mzima wa shughuli hiyo Mratibu wa Takwimu mkoani Mara, Ramadhani Mbega alisema kuwa mpaka sasa taarifa alizozipata kutoka sehemu mbalimbali mkoani Mara zinaashiria zoezi kwenda vizuri.
Alisema matatizo madogo ambayo yalikuwepo kama vifaa, picha kwa makarani kama utambulisho yametatuliwa na hivyo zoezi zima kuendelea kama lilivyopangwa.
“Kulikuwa na matatizo madogo hasa vifaa, picha kwa makarani lakini kwa sasa hali hiyo imerekebishwa na wanaendelea na zoezi vizuri” alisema Mratibu huyo.
Aidha katika maeneo ya Mbugani na Visiwani, Mbega alisema kuwa zoezi hilo limeendelea Vizuri kutokana na maandalizi yaliyokuwe hapo awali na wananchi wa maeneo hayo kuhamasishwa na kupewa elimu ya kutosha juu ya shughuli za sensa na makazi.
Mbali na maeneo hao Mbega alisema kuwa kuna baadhi ya maeneo ambapo viongozi wa vijiji na vitongoji walikuwa wanalalamika juu ya maalipo yao na kuongeza kuwa malipo hayo yanatolewa kwa awamu kama ilivyoagizwa
Kwa sababu hiyo Mratibu huyo wa Takwimu mkoa wa Mara aliwataka wananchi wote wa Mkoa wa Mara kuendelea kujitokeza katika zoezi hilo kwani kwa kufanya hivyo wataisaidia Serikali katika kupango mipango ya Maendeleo kwa wananchi.
“Ya kikubwa mimi naomba wananchi waendelee kujitokeza katika seku zilizosalia ili tukamilishe zoezi hili vizuri kabisa kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imesaidia miapango ya Maendeleo kwa nchi yetu,” aliongeza Mbega
Mbali na kauli hiyo ya Mratibu wa Takwimu mkoani Mara, Ramadhani Mbega, baadhi ya wananchi ambao wamepata nafasi ya kuongelea zoezi hilo walisema kuwa mwenendo mzima wa zoezi la Sense zi mbaya ingawa kuna baadhi ya Maeneo uelemishaji unaonekana kuwa mdogo
“Mimi naona zoezi linaenda vizuri ingawa kuna baadhi ya maeneo hali si nzuri sana kutokana na hamasa kuwa ndogo maeneo hayo” Alisema Juma Omary mkazi wa Kamnyonge mjini Musoma
Hivi karibu akizindua zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Mara, John Gabriel Tuppa ambaye pia ni Mwenyekiti wa katika ya zoezi hilo mkoa wa Mara alisema kuwa zoezi hilo halipaswi kuunganishwa na masuala ya dini kwani lengo la Serikali siyo kujua idadi ya waumini hapa nchini.
Alisema ni vyema watu wakaliunga mkono zoezi hili kwa asilimia kubwa ili Serikali katika mipango yake iweze kufanikisha kufikisha Maendeleo kwa Wananchi.
www.mwanawaafrika.blogspot.com