
Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa akitoa mada wakati wa semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa waajiri wa makampuni na mashirika mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Seaescape, Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam leo.
Mgeni Rasmi Prof. Betria Mapunda akiwa katika picha ya Pamoja na Waajiri pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF leo katika Semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika Katika Ukumbi wa Seascape Hotel Mbezi Beach Jijini Dar.
Baadhi ya Waajiri kutoka Mashirika na makampuni mbalimbali wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wafanayakazi wa Mfuko Wa Pensheni wa PPF.
Majaliwa E Mkinga, Mchambuzi na Mtengenezaji wa Mifumo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akielezea jinsi PPF ilivyotengeneza mfumo wa kupata taarifa za wanachama kupitia simu aina za Smartphone na kuutaja mfumo huo kuwa ni PPF TAARIFA App ambayo mteja ataweza kuiweka katika simu yake ya mkononi.
Baadhi ya waajiri wakielekeza kuhusu jinsi ya kuweka mfumo wa PPF Taarifa katika simu zao za Smartphone leo katika semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Seascape hotel Mbezi beach Jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa akiwaelezea waajiri waliohudhuria semina iliyoandiliwa na mfuko wa pensheni wa PPF leo jinsi kanuni mpya inavyofanya kazi kwa wanachama ili kuweza kupata mafao yao kutoka mfuko wa pensheni wa PPF.