SEMA Kutumia Milion 396 Kuweka sawa Mazingiza ya Shule Iramba

DSC02082

Meneja wa shirika la SEMA, Ivo Manyanku, akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba. Kulia mwenye miwani ni mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda.

Na Nathaniel Limu, Iramba

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Sustainable Environment Management Action (SEMA),linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 396 milioni kugharamia utekelezaji wa mradi wa usafi mashuleni na mazingira kwa ujumla,katika shule saba ba kata saba za wilaya ya Iramba.

Fedha hizo ni ufadhili kutoka shirika la WaterAid Tanzania.

Hayo yamesemwa na meneja wa SEMA,Ivo Manyanku, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingirav nchini, iliyofanyika katika kijiji cha Tulya wilayani Iramba.

Alitaja baadhi ya malengo ya mradi huo, kuwa ni pamoja na kuhamasisha na kuelimisha wanafunzi na jamii kwa jumla namna bora ya kunawa mikono.

DSC02101

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo dunia na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika kimkoa katika kijiji cha Tulya wilayani humo.

“Pia kuwaelimisha wanafunzi wa kike waliopevuka (kuvunja ungo) njia bora zitakazowasaidia kuwa wasafi kipindi chote cha siku zao za hedhi”,alifafanua Ivo na kuongeza kwa kusema;

“Shughuli zingine ni ujenzi wa vyoo bora na kuwahamasisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kuvitumia kikamilifu.Tutawaelimisha na kuwaahamasisha kunawa mikono pindi wanapotoka chooni kujisaidia”.

Kwa upnde wake afisa afya wa wilaya ya Iramba,Yohana Dondi,alisema kuwa wilaya ya Iramba ina kaya zenye vyoo bora ni aslimia 42,vyoo kubalika 52,vyoo visivyokubalika asilimia 18 na bila vyoo,ni aslimia sita.

Kwa mujibu wa afisa huyo,nchi zinazoendelea,asilimia 70-80 ya maradhi yote,yanasababishwa na maambukizi yatokanayo na vinyesi,hivyo kuwa ni kisababishi namba moja cha vifo.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu,ni Choo bora na mikono safi kwa afya bora,heshima na usawa”.

DSC02092

Spider man kutoka Temeke jijini Dar-es-salaam akitoa burudani ya kutembea juu ya waya kwenye hafla ya uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini iliyofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.

DSC02060

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda (wa nne kutoka kushoto) akitoa maelekezo juu ya ujenzi wa choo bora cha shule ya msingi Tulya.Wa tatu kushoto ni meneja wa shirika la SEMA,Ivo Manyanku.

DSC02075

Baadhi ya wakazi wa kata ya Tulya,waliohudhuria uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.(Picha zote na Nathaniel Limu).