Mshindi wa gari wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo, Amin Joseph Maro akiingia ndani ya gari yake aina ya Ford Figo baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries, Ephraim Mafuru, hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine Tengia, wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Allan Chonjo, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager sambamba na Wanahabari.
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries, Ephraim Mafuru akimkabidhi kadi ya gari mshindi wa gari wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo, Amin Joseph Maro kwenye hafla fupi iliyofanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine Tengia wakiwemo Wanahabari ndugu jamaa na marafiki.
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries, Ephraim Mafuru akimkabidhi funguo ya gari lake mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo, Amin Joseph Maro kwenye hafla fupi iliyofanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine Tengia wakiwemo Wanahabari ndugu jamaa na marafiki.
Mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo, Amin Joseph Maro akifurahia zawadi hiyo na Mama yake Mzazi ambaye pia alikuwepo kulishuhudia tukio hilo lililofanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma.
Baba yake Mzazi Mzee Augustine Tengia akizungumzia furaha alionayo mbele ya Wanahabari mara baada ya mtoto wake kujishindia gari mpya aina ya Ford Figo kupitia promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyokuwa ikiendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.