*Ni mkatanba wa miaka mitatu mfululizo
KAMPUNI ya Bia Serengeti (SBL) leo imeingia mkataba wa mitatu na Shirikisho la Mipira wa Miguu Tanzania (TFF) wa thamani ya shilingi bilioni 2.1 ambao unaifanya kuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa -Taifa Stars.
Hii ni mara ya pili kwa SBL kuiunga mkono timu ya taifa baada ya kampuni hiyo kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu ilipoidhamini timu hiyo kati ya mwaka 2008 hadi 2011.
Katika makubaliano hayo ambayo yalisainiwa leo na pande hizo mbili na Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie na Rais wa TFF Jamal Malinzi, kampuni ya SBL itapata fursa ya kutanga biashara yake wakati wa mechi zote za Taifa Stars za nyumbani na ugenini.
Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo Bi Weesie alisema uamuzi wa kampuni hiyo wa kuidhamini timu ya taifa unatokana na sera ya SBL ya kusaidia kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo.
ga mkono sekta ya michezo nchini na kubainisha kwamba michezo sio tu inaburudisha bali pia inaunganisha mashabiki na pia ni chanzo cha kipato kwa vijana.
“SBL inaona fahari kuidhamini timu yetu ya taifa kwa mara nyingine. Tumechukua hatua hiii kwa kuwa tunaelewa mchango wa sekta michezo katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha tunaamini kuwa udhamini wetu utachangia kukuza vipaji vya vijana wetu pamoja na kuleta hamasa kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya taifa,” alisema Weesie.
Kwa upande wake, Rais wa TFF aliishukuru SBL kwa kukubali kuidhamini Taifa Stars jambo ambalo alisema litasaidia katika kufanikisha maandalizi mazuri na ushiriki kikamilifu wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali, ndani nan je ya nchi.
“Udhamini wa SBL umekuja kwa wakati mwafaka, wakati ambapo timu yetu ya taifa ipo katika hatua za maandalizi kwa mashindano ya kikanda na kimataifa,” alisema Malinzi.
Hafla ya kusainiwa kwa udhamini huo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe ambaye alitoa wito kwa kampuni zingine na watu binafsi wenye mapenzi na michezo kujitokeza na kutoa michango ya hali na mali ili kuendeleza sekta hiyo.