
Mtoa Mada Mkuu katika Marketer’s Night Out iliyoandaliwa na kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd, Dk. Wale Akinyemi akizungumza na maOfisa masoko waliohudhuria katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam, Maofisa Masoko kutoka makampuni mbalimbali wamehudhuria katika usiku huo na kupata uzoefu katika mada mbalimbali zilizowasilishwa na wataalam.

Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries, Steve Gannon akizungumza. Picha zingine juu waliokaa ni baadhi ya maofisa masoko kutoka makampuni mbalimbali wakijumuika katika hafla hiyo.

Kutoka kushoto ni Steve Gannon Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Ephraim Mafuru wakifuatilia mada ya Dk. Wale Akinyemi.


Juu ni waimbaji wa bendi ya Banana Zoro ‘The B Band’, pichani juu ni katikati ni Mkurugenzi na Muimbaji wa Bendi The B, Banana Zoro akifanya vitu vyake jukwaani wakati wa usiku wa maofisa masoko uliofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip.

Wakuu wa Vitengo vya masoko kutoka makampuni mbalimbali wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Dk. Wale Akinyemi.