SBL wamleta bingwa wa ‘cocktail’ Tanzania

Mtaalam wa kuchanganya vinywaji vikali duniani kulia, KENJI JESSE akifafanua jambo kwa mtangazaji wa EATV namna ya kuchanganya vinywaji mbalimbali na kuwa kinywaji cha aina

Na Japhet ole Lengine

YULE bingwa wa kuchanganya vinywaji vikali duniani maarufu kama (cocktail) kutoka London Uingereza, Kenji Jesse, sasa ametua hapa nchini kwa udhamini ya Kampuni nya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji cha Smirnoff kinachosambazwa na kampuni hiyo.

Mtaalam huyo wa kuchanganya vinywaji vikali vya aina mbalimbali na kutengeneza kinywaji chenye ladha ya kipekee, ameendesha semina maalum kwa watoa huduma ya vinywaji na jinsi gani wanawe za kuhudumia wateja wao.

Akizugumza waandishi wa habari na wajasiriamali mbalimbali wanaojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa vinywaji hivyo katika semina ya mafunzo mafupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji bora cha Smirnoff.

Jesse amesema kampuni zinazotengeneza vinywaji vikali vinaongoza katika kulipa kodi na vinaongoza katika kutoa misaada mbalimbali kwa jamii inayoizunguka kote duniani.

Jesse aliongeza kuwa maeneo mengi duniani ya naonekana kuweka kipaumbele katika mashirika na makampuni mengine na kusahau umuhimu wa kampuni zinatengeneza pombe kwasababu hiyo yeye ameamua kutembea duniani kote kuendesha semina anuai kuhusiana na jinsi ya kuchanganya vinywaji na namna ya kumhudumia wao.

Akielezea kwa undani faida za uchanganywaji wa vinywaji vikali, Jesse amesema kuwa kama watu wangejua namna ya kuchanganya basi soko la vinywaji vikali lingekuakwa kasi kubwa hali ambayo ingeongeza kipato kwa taifa na kwwa jamii kwa ujumla.