Samuel Sitta Achaguliwa Mwenyekiti wa Kudumu Bunge la Katiba

Samuel Sitta

Samuel Sitta

Na Mwandishi Wetu

MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba. Sitta amechaguliwa muda huu baada ya kumshinda mgombea mwenzake wa nafasi hiyo, Hashim Rungwe Sipunda aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Thomas Kashillilah alisema Samuel Sitta amemshinda Rungwe baada ya kujipatia jumla ya kura 487, huku mwenzake akiambulia kura 69. Dk. Kashillilah alisema jumla ya wapiga kura wote walikuwa 563 na kura 7 ziliharibika ikiwa ni sawa na asilimia 1.2. Habari zaidi juu ya uchaguzi huo zitakujia muda si mrefu.