Samsung Yahamasisha Kulindwa kwa Haki za Mteja Tanzania

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania, Bw. Sylvester Manyara  katikati akizungumza na mmoja wa washindi wa Pambika na Samsung.

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania, Bw. Sylvester Manyara katikati akizungumza na mmoja wa washindi wa Pambika na Samsung.

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania, Bw. Sylvester Manyara akifafanua jambo kwenye droo ya Pambika na Samsung leo.

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania, Bw. Sylvester Manyara akifafanua jambo kwenye droo ya Pambika na Samsung leo, Jumla ya washindi 15 wamezawadiwa bidhaa mbalimbali toka Samsung katika droo ya nne mara baada ya kununua bidhaa halisi za Samsung na kuisajili.

Jopo linaloendesha bahati nasibu ya Pambika na Samsung likitafuta washindi.

Jopo linaloendesha bahati nasibu ya Pambika na Samsung likitafuta washindi.

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania, Bw. Sylvester Manyara  katikati akizungumza na mmoja wa washindi wa Pambika na Samsung.

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania, Bw. Sylvester Manyara katikati akizungumza na mmoja wa washindi wa Pambika na Samsung. Jumla ya washindi 15 wamezawadiwa bidhaa mbalimbali toka Samsung katika droo ya nne mara baada ya kununua bidhaa halisi za Samsung na kuisajili.

SHERIA za kulinda haki za mteja zinampa uwezo mtu yeyote haki ya kudai fidia juu ya bidhaa ambao haiendani na thamani ya kiasi alichotoa au bidhaa ambayo haina kiwango. Sheria hizi zimetungwa ili kuwakabili wauzaji wa bidhaa na watoa huduma kuwajibika katika biashara zao moja kwa moja pale wanapofanya biashara kinyume na sheria zilizopo.

Katika harakati za kulinda wateja wake, kampuni ya Samsung imezindua mfumo maalum wa kuangalia uhalisia wa bidhaa zake zinunuliwazo unaojulikana kama ‘e-warranty’ unaomuwezesha mteja kugundua simu halisi za Samsung kwa kupitia namba maalum za kimataifa za kujua mahala simu imesajiliwa yaani namba za IMEI. Huduma hii ya dhamana ya ziada inatoa ofa kwa wateja wote wa Samsung nafasi ya kipekee ya kuangalia uhalisia wa bihdaa.

Moja kati ya changamoto kubwa katika soko la simu nchini Tanzania leo hii ni kwamba soko limegubikwa na bidhaa feki, mbovu na zisizo na dhamana. Ni vigumu kwa mteja kujua ipi bidhaa halisi na ipi sio. Samsung inaamini kwamba mteja anatakiwa awe na huduma ambayo itampa fursa ya kuangalia uhalisia wa simu yoyote atakayonunua na ndio maana wao wamekuja na huduma hii muhimu katika kulinda haki ya mteja.

Huduma hii ya dhamana inafanya kazi katika nchi 15 tu za Africa ambapo ili mteja aweze kupata huduma hii itakayompa dhamana ya miaka miwili atatakiwa kujisajili kwa kutuma tarakimu 15 zilizo nyuma ya simu hiyo. Nchi nyengine yenye huduma kama hii ni Afrika ya Kusini, Nigeriia, Kenya, Ghana, Sudan, Ethiopia, Namibia, Zambia, Mauritius, Uganda, Ivory Coast, Angola, Botswana, and Msumbiji.
Katika kuhakikihsa elimu ya huduma hii muhimu kwa Watanzania inasamabaa kwa haraka zaidi, Samsung Tanzania ilizindua promosheni kabambe katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka inayojulikana kama Pambika na Samsung itakayodumu mpaka Desemba 23, 2013. Promosheni hiyo inalenga kuhamasisha wateja kununua bidhaa halisi na kuzisajili kasha kuzawadiwa katika droo za kila wiki na droo kubwa ya mwisho wa promosheni.

Akizungumza wakati wa droo ya nne ya kila wiki ya Pambika na Samsung, Bw. Sylvester Manyara Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania amesema kwamba Samsung inadhamira ya dhati katika kulinda haki za mteja na kumlinda kutokana na bidhaa feki ambazo zipo kila kona kwa sasa. “Wateja wote wana haki ya kujua kuhusu umiliikaji wa bidhaa zao wakati wa kununua. Ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa Samsung tunajitolea kulinda haki za wateja kwa kuwapa wateja wetu jukwaa la kufurahia uamuzi wao wa kununua bidhaa halisi” alisema Bw. Manyara.

Droo ya nne imetoa washindi 15 wengine ambao wamepokea bidhaa mbalimbali toka Samsung kama Jokofu lenye dhamana ya miaka 10 toka Samsung, Luninga ya LED 32’, Kompyuta mpakato, Jiko la kupashia chakula, Muziki wa nyumbani pamoja na deki za DVD toka Samsung. Jumla ya wateja 60 kutoka mikoa mbalimbali tayari wameshapatikana. Jumla ya wateja 15 wamejishindia zawadi mbalimbali leo zikiwemo TV kubwa ya kisasa ya Samsung, Mashine ya kufulia, mashine ya kupasha moto vyakula na deki za DVD za kisasa kutoka kampuni ya Samsung.

Hii ni aina nyengine ya huduma iliyoletwa na Samsung ili kulinda haki za wateja na kuwalinda kutokana na madhara ya kununua bidhaa feki. Pambika na Samsung inawazawadia wale wote wanaonunua na kusajili bidhaa halisi za Samsung kila wiki kabla ya kutolewa kwa zawadi kubwa ya gari jipya la Mitsubishi Double Cabin itakayokuwa imesheheni bidhaa zote zinazotoka kila wiki ambapo mteja mmoja mwenye bahati atajinyakulia hapo Desemba 23, 2013.