KAMPUNI ya Samsung imezinduwa rasmi duka kubwa na kituo chake cha huduma kwa wateja lililopo barabara ya Sokoine Mjini Arusha. Uzinduzi huo utawawezesha wateja wake wote mkoani Arusha kupata huduma stahiki na bidhaa halisi za Samsung. Kituo hicho cha kwanza kuzinduliwa mkoani Arusha na kampuni hii yenye idadi kubwa ya wateja wa vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni.
“Mtazamo wa maisha ya wateja hubadilika kwa kasi kubwa na kuwafanya kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma bora. Kama kampuni kubwa inayoongoza kuwa navifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni, Samsung imefanya juhudi kubwa kuhakikisha inatimiza mahitaji ya wateja wake wote Afrika. Mkoawa Arusha hutegemea sana biashara kwani una wakazi toka jamii mchanganyiko. Hivyo katika Afrika Mashariki, Arusha ni kitovu cha wageni toka nchi mbalimbali ulimwenguni.
Kampuni ya Samsung inaimani kubwa kwamba kituo cha huduma kwa wateja kitatoa ushirikiano mzuri na kuboresha uhusiano kwa wateja wake mkoani Arusha. Kwasababu Arusha ni kituo kikuu cha safari nchini Tanzania,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hii nchini Tanzania, Bw. Seo.
Mbali na kuuza simu za mkononi na bidhaa za kielektroniki, duka hilo jipya la Samsung litatoa huduma za ziada kwa wateja wake. Hii ni pamoja na kuwapa wateja wake watakaojisajili na uduma ya e-warranty (dhamana) usaidizi wa kiufundi bila malipo kwa kipindi cha miaka miwili.
Mpango huu utawanufaisha wateja wa Samsung watakaosajili bidhaa zao kupitia Simu. Huu ni mchakato utakaofanyika kwa kutuma namba ya IMEI kwenda 15685. Baada ya kufanya hivyo wateja watanufaika na msaada wa kiufundi kwa kipindi cha miaka miwili sambamba na kujipatia nafasi ya kushinda bidhaa mbalimbali za Samsung.
Katika kusherehekea uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja ambacho kinawasogezea wateja wake huduma karibu, kampuni hii kubwa duniani inawaletea habari njema wakazi wa Arusha kwa kutoa punguzo kubwa la bei za bidhaa zake. Kwenye kipindi hiki cha ufunguzi bidhaa zitakazo kuwa na punguzo la bei ni pamoja na Luninga, feni, majokofu na vifaa vya nyumbani. Bila kuwa sahau wateja wake wa simu, vifurushi vya intaneti na zawadi za T-shirts zitatolewa kwa ajili ya wanunuzi wa simu aina ya Galaxy Trendlite.
Kwa sasa nchini Tanzania kampuni ya Samsung inamaduka na vituo vya huduma kwa wateja katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam na inamipango kabambe kuongeza huduma zake mikoa mingine. Duka hili na kituo chake cha huduma kwa wateja vitatoa huduma siku za wiki yaani Jumatatu – Ijumaa kuanzia saa 9.30 asubuhi hadi 5.00 jioni kwa Jumamosi ni kuanzia saa 9.30 asubuhi hadi 1.00 mchana, litafungwa siku za Jumapili na Sikukuu.