Samatta Apongeza SBL kwa Udhamini wa Taifa Stars

Mchezaji soka wa kimataifa wa Tanzania na Nahodha wa Taifa stars Mbwana Sammata akizungumza  na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema m mwishoni  wa wiki iliyopita kuhusu maandalizi yao ya kucheza na Lesotho katika mkutano na waandishi uliofanyika katika makao makuu ya TFF .

 
  
Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo uliofanyika mapema mwishoni mwa wiki iliyopita.
Na Mwandishi Wetu 
 
 MCHEZAJI soka wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Sammata ameihakikishia kampuni ya Bia ya Serengeti  ambayo ni wadhamini wa timu ya taifa Taifa Stars kwamba wachezaji wa timu hiyo watajituma  ili kuhakikisha kuwa wanashinda mechi zote  walizopangiwa kwenye ratiba.
 
 
Samatta ambaye ni nahodha wa timu hiyo ya taifa  alitoa hakikisho hilo jijini Dar es Salaam jana  katika mkutano wa waandishi wa habari  ulioandaliwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kuhudhuriwa na Meneja Masoko wa SBL, Nicholus Machugu. Mkutano huo ulijadili mechi kati ya Taifa Stars na Lesotho  timu ambayo Stars inatarajiwa kucheza nayo  katika mashindano yajayo.
Alithibitisha kuwa timu hiyo haitaiangusha SBL katika  mechi zake kwa kuwa kampuni hiyo imeonesha  kuithamini kutokana na udhamini wake kwa timu hiyo.
 
Aidha alitoa wito kwa wachezaji wenzake  kuhakikisha kuwa wanajiweka vizuri  kkwa ajili ya mechi hizo  ili waweze kuingia na kutambuliwa katika ramani ya soka barani Afrika.  Samatta ambaye hivi sasa  anafanya shughuli zake kama  mchezji wa kulipwa nchini Ubeljiji aliinga jijini Dar es Salaam Jumatano ya wiki hii ili kuungana na wachezaji wenzake wa timu ya taifa  kwa ajili ya mechi ya duru ya kwanza ya kufuzu mashindano Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Duru ya pili ya mashindano hayo  itafanyika Januari 2018 na mechi ya fainali inatarajiwa kufanyika  kufanyika Cameroon mwka 2019.
 
Kwa upande wake Kocha wa Timu hiyo Salum Mayanga  alisema kwamba timu yake  imejitayarisha sawasawa kwa ajili ya mechi zote na kuongeza kuwa  mazoezi ya timu hiyo iliyoyafanya walipokuwa Alexandria, Misri walikokuwa hivi karibuni hivi karibuni  yaliwapa  mwanga na ana matarajio makubw kwamba timu hiyo  itashinda mechi zote.
 
 Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ni mashindano ni mashindano makubwa ya kimatiafa  barani Afrika. Mashindano hayo yalianzishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1957.  Kuanzia mwaka 1967, yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili. Wanachama wa Mashirikisho ya Soka ya FIFA ndio walio na sifa za kushiriki mashindano hayo.