Salamu za Valentine Kutoka TGNP

Salamu za Valentine Kutoka TGNP

SALAAM za ‘Valentine’s Day” kutoka TGNP!
Tuna kauli mbiu yetu ya kuadhimisha valentine mwaka huu na tunahamasisha watu wote (sio wapenzi tu) kupendana bila ubaguzi, ukatili, unyonyaji, na unyanyasaji wa aina yoyote. Valentine iwe kichocheo cha kukua kwa upendo, umoja na mshikamano kati yetu na kuimarisha mahusiano yetu.

TGNP tunahamasisha mgawanyo sawa wa rasilimali kwa mtazamo wa Kijinsia, tunaamini kama kuna upendo wa dhati miongoni mwetu kuanzia viongozi wa juu kutakuwepo na usawa na kila mmoja wetu atafaidi keki ya Taifa.

Kila mmoja ampende mwenzake bila kikomo na upendo usiwe wa siku moja (Februari 14) pekee. Tunataka upendo wa kudumu kwa kila mmoja, wazazi, watoto, Vijana, viongozi, na wanajamii wote kwa ujumla.

Tunawatakia kila la kheri na siku njema ya wapendanao!