Umoja wa watanzania waishio nchini Ujerumani unatoa mkono wa pole na rambirambi kwa ndugu jamaa na marafiki wote waliopatwa na maafa kutokana na ajali ya meli ya MV SKAGIT iliyotokea eneo la Chumbe Zanzibar siku ya tarehe 18.07.2012
Umoja huo umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo.Aidha umoja huo unaungana na watanzania wote katika kipindi hiki cha majonzi na maombolezo.
.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU UBALIKI UMOJA WA KITAIFA
imetolewa na Mfundo Peter Mfundo
Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio Ujerumani (UTU)