Salam za Rambirambi kutoka Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimpa pole Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati walipokutana katika viwanja vya Maisala, walipofika kutembelea mabanda ya kupokelea miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice Islanders Septemba 10.

WATANZANIA tunaoishi ujerumani tumesikitishwa sana na habari mbaya ya ajali ya meli iliyotokea 10.09.11 katika bahari ya hindi katikati ya visiwa vya Pemba na Unguja nchini Tanzania. Ajali hii ni pigo na msiba mkubwa kwa Taifa letu. Salam za rambirambi ziwafikie Familia za wafiwa, Viongozi wa Tanzania, na watanzania wote kwa ujumla.

Umoja wa watanzania ujerumani (UTU) kwa masikitiko makubwa tunaungana na wanafamilia, na taifa zima katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa vyombo mbali mbali kwa jitihada zake za kuokoa maisha na kusaidia kwa namna moja au nyingine katka janga hili kubwa kwa Taifa
Tunaomba kwa mwenyezimungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi amen

— kny ya UTU
Mfundo Peter Mfundo
Mwenyekiti

Schwindstrasse 1
63739 Aschaffenburg
Germany
Res: +4960216253026
Cell: +491733 779720
Cell +491734297997