Saidi Kuboresha Maisha ya Albino kwa Kupiga Kura Hii…!

Saidi Kuboresha Maisha ya Albino kwa Kupiga Kura Hii...!

SHIRIKA linalojibidisha na kutetea na kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Under the Same Sun, (UTSS) limeteuliwa kushindania  Tuzo ya Haki za Binadamu ijulikanayo kama “Tulip” itolewayo  nchini Uholanzi.  Iwapo UTSS watashinda tuzo hiyo, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mapinduzi makubwa  katika uboreshaji wa maisha ya watu  wenye ulemavu wa ngozi.  Shiriki kwa kupiga kura ili UTSS washinde Tuzo hii na kulinda ndugu zetu wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania kwa kupiga kura hapa chini na kusambambaza tarifa hizi kwa taasisi na watu mbalimbali.

Kwa kupiga kura hiyo bofya; www.humanrightstulip.nl