Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza tija na uzalishaji kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe, Iringa na Mbeya, Mfuko Kichocheo wa SAGCOT yaani SAGCOT CATALYTIC TRUST FUND tarehe 12 Agosti 2016 umesaini makubaliano na Shirika la Bothar kutoka nchini Ireland ambalo linajihusisha na kutoa misaada mbalimbali inayolenga kutoa fursa kwa familia zenye kipato cha chini kuweza kuboresha maisha yao kupitia uwekezaji wa shughuli zinazowaletea kipato hususani kaya zinazojishughulisha na ufugaji.
Katika makubaliano hayo jumla ya Ng’ombe wa kisasa 630 wanatarajiwa kuingizwa nchini katika kipindi cha
miaka mitatu. Ng’ombe hao watagawiwa kwa wafugaji walioandaliwa chini ya miradi inayotekelezwa na Mfuko huo, Aidha wafugaji watahakikishiwa masoko pamoja na huduma mbalimbali za mifugo kupitia wataaalamu wa
Halmashauri husika.

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT Bw. John. J. Kyaruzi ( kushoto) akisaini makubaliano na Muasisi wa Bothar Bw. Peter Ireton.
Mkurugenzi wa huduma za nje ya Nchi wa Bothar, Dk. Bernard Muyeya akitoa maelezo kwa wajumbe namna shirika hilo linavyotoa huduma zake.