Safari ya mkutano wa wahariri na matukio katika picha


Safari ilianzia hapa (Dar es Salaam) kwa kutumia mabasi ya kisasa ya Kampuni ya Metro kuendelea mkoani Arusha. “Haina majotrooooooooooo” ni burudani kwenda mbele.


Baadhi ya wahariri na wanamsafara mzima wakipata picha za kumbukumbu kabla ya kuivuka ardhi ya Jiji la Dar es Salaam.


Baadhi ya wahariri wakijuliana hali huku safari ikiendelea. Haikuwa ajabu mtu kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine ilimradi usihatarishe amani kwa wengine.


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda (aliye simama katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya wahariri huku safari ikiendelea.


Hapa magari akiwa yanapumua baada ya safari ndefe kabla ya kuingia Moshi Mjini.


Baadhi ya wahariri wakila pozi katikati ya safari baada ya kushuka kwenye mabasi kunyoosha miguu. Hureeeeeeeeeeeeeeee…….wengine wamekolea siunajua Serengeti bwana..!


Hapa basi moja lilikuwa na ‘walokole’ yakheee wakalazimika kutupunguzia The Serengeti kwenye basi la pili, wadau wakasema kwa pamoja; “Hainamajotrooooo…hamisheni kreti zoteee”.