Safari ya Lowassa Ikulu 2015 Yazidi Kunoga, Vijana Wamshawishi…!

Lowassa akipeana mikono na baadhi ya vijana walioandamana hadi makazi yake mjini Dodoma kumshawishi kugombea urais 2015.

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais. 

Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu.Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura.

 
 

 Wanafunzi hao zaidi ya 300 walifika nyumbani kwake hapo majira ya saa sita mchana na kuzungumza nae na kufikisha salamu zao ikiwa ni pamoja na kumchangia fedha za kuchukulia fomu.
 Walibeba na mabango yaliyo na jumbe mbalimbali
 Bodaboda nao walifika eneo hilo
Sehemu tu ya umati uliofika nyumbani hapo kwa Lowassa hii leo.