Sababu za Jengo la NSSF Kuungua Zatajwa…!

Sehemu ya Jengo la NSSF eneo la Akiba jijini Dar es Salaam likiwaka moto ghorofa ya tano.

Sehemu ya Jengo la NSSF eneo la Akiba jijini Dar es Salaam likiwaka moto ghorofa ya tano.

WATU walioshughudia Jengo la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) eneo la Akiba kuungua moto jana wamwtaja sababu zilizosababisha kuzuka kwa moto huo ambao ulianza kuwaka katika moja ya ofisi zilizopanga katika jengo hilo jioni.

Akizungumza na dev.kisakuzi.com mmoja wa wafanyakazi katika jengo hilo ambalo lina ofisi mbalimbali za Serikali na kampuni binafsi zilizopanga alisema moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme iliyoibuka ndani ya ofisi ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii ambaye hakuwepo ofisini muda huo.

“…Taarifa za awali zinaonesha chanzo ni shoti ya umeme iliyoanzia katika ghorofa ya tano kwenye ofisi ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii ambaye amesafiri…ilianza kuwaka majira ya saa kumi na mbili jioni, hakuna aliyejeruhiwa lakini vitu ndani ya ofisi hizo vimeungua,” alisema shuhuda huyo akizungumza na mwanahabari wetu.

Jengo hilo mali ya NSSF ambalo linawapangaji mbalimbali lilishika moto jana na kuzua tafrani kwa wafanyakazi katika ofisi hizo ambao baadhi yao muda huo walikuwa wakitoka kazini, hata hivyo kikosi cha zimamoto kilifika na kuanza kuuthibiti moto huo.