Ruvuma Yazinduwa Kampeni ya Bwela Kuni na Wimbo Maalum

Mratibu wa kampeni ya Bwela Kuni, Raymund Mhenga (wa kwanza kushoto) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia Kampeni ya Bwela Kuni zinazotarajia kunadi fursa anuai zilizopo katika mkoa wa Ruvuma.

Mratibu wa kampeni ya Bwela Kuni, Raymund Mhenga (wa kwanza kushoto) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia Kampeni ya Bwela Kuni zinazotarajia kunadi fursa anuai zilizopo katika mkoa wa Ruvuma.

Mhamasishaji wa Utalii na Maliasili katika Kampeni ya Bwela Kuni, Bakari Likapo akizungumza katika mkutano na wanahabari.

Mhamasishaji wa Utalii na Maliasili katika Kampeni ya Bwela Kuni, Bakari Likapo  (wa pili kulia) akizungumza katika mkutano na wanahabari.

Produza C9 (katikati) akizungumza na wanahabari kuzungumzia Kampeni ya Bwela Kuni na Wimbo Maalum aliouandaa kuzungumzia Mkoa wa Ruvuma.

Produza C9 (katikati) akizungumza na wanahabari kuzungumzia Kampeni ya Bwela Kuni na Wimbo Maalum aliouandaa kuzungumzia Mkoa wa Ruvuma.

Baadhi ya vijana na washiriki wa Kampeni ya Bwela Kuni katika mkutano na wanahabari.

Baadhi ya vijana na washiriki wa Kampeni ya Bwela Kuni katika mkutano na wanahabari.

Baadhi ya vijana wasanii walioimba wimbo maalum wa Kampeni ya Bwela Kuni unaousifia Mkoa wa Ruvuma wakitoa kionjo cha wimbo huo katika mkutano na wanahabari.

Baadhi ya vijana wasanii walioimba wimbo maalum wa Kampeni ya Bwela Kuni unaousifia Mkoa wa Ruvuma wakitoa kionjo cha wimbo huo katika mkutano na wanahabari.

Baadhi ya vijana na wasanii pamoja na viongozi wa Kampeni ya Bwela Kuni wakiwa katika picha ya pamoja.

Baadhi ya vijana na wasanii pamoja na viongozi wa Kampeni ya Bwela Kuni wakiwa katika picha ya pamoja.

BAADHI ya Vijana kutokea Mkoa wa Ruvuma wakishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wameandaa kampeni maalum ya kunadi fursa anuai zilizopo katika mkoa huo kupitia sanaa ya muziki kwa kuwashirikisha wasanii na vijana wenye vipaji. Kampeni hizo zilizopewa jina la ‘BWELA KUNI’ neno la lugha ya Kingoni lenye asili ya mkoa huo likiwa na maana ya ‘njoo hapa’ zitazinduliwa rasmi mwishoni mwa Septemba, 2014 kwa tamasha kubwa litakalofanyika katika Uwanja wa Maji Maji mjini Songea hivi karibuni.

Akizungumzia na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa kampeni ya Bwela Kuni, Raymund Mhenga alisema kampeni hizo zilizo na lengo la kunadi fursa anuai za uwekezaji zinazopatikana eneo hilo kwa kushirikisha vijana wasanii zitashirikisha makundi anuai ya sanaa ikiwemo sanaa muziki wa kizazi kipya, injili, uigizaji.

“…Hii ni kampeni maalum iliyoanzishwa na vijana wanaotokea na wenye asili ya Mkoa wa Ruvuma wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, wasanii wamuziki wa injili, waigizaji na wasanii wengine wa kada tofauti tofauti kwa madhumuni ya kuamsha ari na hamasa ya wananchi wa mkoa huu na wenye asili ya mkoa huu na Watanzania kwa ujumla kuweza kutangaza sifa za mkoa wetu…,” alisema Mhenga.

Alisema kampeni hiyo pia itatangaza historia ya Mkoa wa Ruvuma, tamaduni za watu wake na fursa mbalimbali zinazopatikana eneo hilo kwenye sekta ya kilimo, utalii, biashara, elimu na uvuvi kupitia sanaa. “…Hii pia itakuwa ni fursa ya pekee kwa wasanii watakaoshiriki kwenye kampeni kuweza kutangaza vipaji vyao na uwezo hivyo kutambulika kitaifa na kimataifa,” alifafanua Mhenga.

Alisema kampeni hiyo kwa kuanza imewaunganisha wasanii vijana wenye asili ya Mkoa wa Ruvuma na kuandaa wimbo unaojulikana kama “Bwela Kuni” ambao pia umeandaliwa na Produza mwenye asili ya mkoa huo maarufu kwa jina la C9 Kanjenje na tayari umetolewa kuchochea kampeni hizo.

Aidha Mhamasishaji wa Utalii na Maliasili katika kampeni hizo, Bakari Likapo alisema kampeni hiyo imekusudia kubainisha vivutio na fursa za uwekezaji zinazopatikana katika Mkoa wa Ruvuma ikiwemo vituo vya makumbusho ya taifa (Vita vya Majimaji), Mbuga ya Wanyama Selous, utamaduni wa jamii ya wakazi wa eneo hilo pamoja na kuhamasisha wawekezaji kutumia fursa hizo.

Alisema Mkoa huo una Ziwa Nyasa, upatikanaji wa madini mbalimbali na fursa za kilimo kupitia ardhi yenye rutuba jambo ambalo likitangazwa na wawekezaji kujitokeza linaweza kuchochea kasi ya maendeleo ambayo yatawanufaisha zaidi wananchi wa eneo husika na taifa kiujumla.

Hata hivyo, Likapo aliwataka viongozi wa Serikali na wanasiasa pamoja na wadau wengine wapenda maendeleo kujitokeza na kuunga mkono juhudi hizo za vijana wa Ruvuma na wasanii za kuchochea maendeleo kupitia sanaa ya muziki.

Miongoni mwa wanamuziki vijana 15 ambao wameshiriki kuimba mwimbo wa hamasa ya kampeni ya Bwela Kuni ni pamoja na Herieth Ndosi (toka muziki wa injili), Single J, G Luck, Cammy Bway, Roby Songea, Gemy Rymez, Fobyone, Bad H Badilika, G Van, Zero Wiz, FM, HDM, Full P, Tony na D Pesa.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com