Ruvu Shooting, Simba Sasa Kucheza Mei 5

Katibu Mkuu, Angetile Osiah


MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe Aprili 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo. Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza
kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.
 
Ligi hiyo inaendelea tena Aprili 26 mwaka huu kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam itakayochezwa
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili, Aprili 28 mwaka huu itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.