Rushwa, Ufinyu wa Demokrasia ni Tishio kwa EAC

Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki


 
Na Isaac Mwangi, EANA Arusha

MKUTANO wa pili wa Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika Bujumbura, Burundi umebaini kwamba demokrasia ndogo, kiwango kikubwa cha rushwa, ukosefu wa haki wa kihistoria pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu, kuwa ni miongoni mwa hatari za kiusalama zinazoikabili kanda hiyo.
 
Akizungumza katika mkutan huo Mkurugenzi wa Taasisi ya Amani na Usalama Afrika, Peter Edobu alitoa wito wa kuimarishwa kwa demokrasia na utawala wa sheria. Alisema kuwa kanda ya EAC inakabiliwa na utofauti katika katiba za kitaifa ikiwa ni pamoja na mifumo dhaifu na inayopingana ya sheria na sera.
 
Matatizo mengine yanayoikabili kanda hiyo aliyataja kuwa ni pamoja na kutokuwepo na umoja katika masuala ya siasa na kukosekana na ukomavu wake katika nchi zote wananchama wa EAC. Sambamba na hayo aliongeza kuna kutoheshimu taaisisi za kisiasa na viongozi wake na pia kuwepo siasa za kikabila na kidini.
 
Edobu alisema nchi zote wanachama zimekuwa zikijihusisha na chagauzi ambazo zimetiliwa mashaka. Mtoaji maoini katika Masuala ya Kijamii wa Tanzania, Jenerali Ulimwngu alisema kuongezeka kwa vitendo vya kutovumilina kidini na ubaguzi ni miongoni mwa changamoto za amani na usalama.
 
Mtaalamu wa Masuala ya Amani na Usalama wa EAC, Leonard Onyonyi alizitaja changamoto nyingine za ndani kuwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, usalama wa chakula,wizi wa mifugo na ujambazi, matumizi ya madawa ya kulevya, uharibifu wa mazingira na ukosefu wa usalama wa taasisi za maji za kikanda.