Mchezaji wa Manchester Wayne Rooney ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa 2015 akitetea tena Tuzo ambayo pia aliizoa mwaka 2014.Hii ni mara ya 4 kwa Rooney kuchukua tuzo hiyo.
Mapema Disemba Uingereza iliyaweka hadharani majina ya Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Nchi yao .
Mwaka 2015 Rooney aliiongoza Nchi yao kufuzu kuingia Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, ambazo zitachezwa huko France Mwezi Juni huku akihakikishia Uingereza itashinda Mechi zao zote 10 za Kundi lao na kuifungia Jumla ya Bao 5 kwa Mwaka 2015 kwa nchia yake
Pia akiivunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Ufungaji Bora katika Historia ya England kwa kufunga Bao 50 Rekodi ambayo iliwekwa na Charlton Mwaka 1968 alipofunga Bao lake la 49.
Wachezaji waliokuwa wanawania Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Mwaka,Joe Hart (Manchester City),Gary Cahill (Chelsea),Raheem Sterling (Manchester City),Wayne Rooney (Manchester United),Harry Kane (Tottenham Hotspur).