RIPOTI YA UCHUNGUZI WA HALI YA ELIMU KIUJUMLA MKOANI LINDI KAZI ILIYOFADHILIWA NA RUZUKU BINAFSI KUTOKA TMF
Aina ya Ruzuku: RUZUKU YA MKOANI
Jina kamili la Mpewa ruzuku: JOACHIM MUSHI
Namba ya Mkataba: TMOG4P01
Kipindi cha Mkataba: 21/04/2009 HADI 21/07/2009
Muda uliotumika kwenye Mkataba: 21/04/2009 HADI 26/05/2009
Kiasi cha pesa kilicho idhinishwa: 561,000.00
SEHEMU A: TAARIFA YA KAZI
Fomu hii ni lazima irudishwe TMF wiki mbili baada ya kumalizika kwa kazi ikiwa na taarifa zifuatazo:
Kifungu 1: Idadi ya Habari na Vyombo vya Habari
Hitaji 1: Orodhesha habari zilizotokana na kazi yako ukionyesha jina la chombo cha habari ambacho kilichapisha au kutangaza kazi yako.
Habari husika Chombo cha Habari ilipotumika
1. Waliofaulu Lindi wakacha kujiunga na sekondari Gazeti la Kulikoni (18/05/2009)
2. Jando, Unyago vyakwaza maendeleo ya elimu Lindi Gazeti la Kulikoni (20/05/2009)
3. Mwamko mdogo wa elimu unazorotesha maendeleo ya elimu mkoani Lindi Gazeti Kulikoni (21/05/2009)
4. Kipato duni, mtazamo hasi, tamaduni potovu zinaathiri elimu mkoani Lindi Gazeti Kulikoni (22/05/2009)
5. Nani kawaloga wazazi hawa hadi kutamani enzi za ujima? Gazeti la Kulikoni (22/05/2009)
6. Maelfu waendelea kuwa mbumbumbu Lindi Gazeti la Kulikoni (25/05/2009)
7. Mikakati ya Mkoa wa Lindi kuboresha elimu Gazeti la Kulikoni (26/05/2009)
TMF inakutaka uwasilishe ushahidi wa kazi yako ya mwisho kwa kutuma nakala za machapisho ya habari au makala ( waandishi wa magazeti) au vipindi vilivyorekodiwa kwenye CD na DVD kuhusu habari au makala zilizotangazwa kwenye luninga na redio. Tafadhali eleza sababu kwa habari ambazo hazikuchapishwa wala kutangazwa kwenye chombo chochote kile:
Habari ambazo hazikuchapishwa katika uchunguzi wote ni zile vyanzo vyake vilitoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambapo nilifanya mahojiano na Kaimu Ofisa Tawala wa Mkoa, Bw. Abdul Dachi ambaye mara baada ya kufanya mazungumzo naye kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Bw. Said Sadick, nikiwa tayari nimerudi Dar es Salaam alinipigia na kuniomba nisitumie taarifa zake kwa maelekezo ya viongozi wake wa juu.
Baada ya kuwasiliana na Mentor wangu na alinishauri kuwa hakuna ubaya endapo nitazitumia taarifa zake lakini bila kumtaja muhusina na ziwe zimetoka ofisi ya mkoa kiujumla.
Ofisa huyo aliniambia amepewa maelekezo nimsubiri Mkuu wa mkoa mwenyewe hadi atakapo rudi mkoani Lindi hali ambayo nisingeweza kukaa kutokana na ratiba yangu na bajeti ya kazi. Hata hivyo, hali hiyo haikunikwamisha kitaarifa kwani sehemu kubwa ya taarifa nilikuwa ninayo hadi muda huo.
Hitaji 2: Orodhesha vyombo vingine vya habari vilivyotumia habari zako mbali na chombo ulichokusudia awali
Chombo cha Habari1
Namna habari ilivyotumiwa na lini
Thisday Lindi Region to track 1,658 students for failing to report for form one classes
Hitaji 3: Orodhesha mtazamo na maoni uliyopata kutoka kwa wasomaji/wasikilizaji na watazamaji kuhusu habari yako
Maoni Mtazamo
Mrejesho Aina ya mapokeo/Mtazamo: chanya/hasi/maswali Ulivyopata mrejesho:
Barua/ujumbe mfupi wa simu/Simu/barua pepe
Jinsia ya aliyekupa mrejesho
1. Mr. Mushi Joachim naomba wape walimu pole hali hiyo ilinikuta na mimi miaka ya 1970 huko huko Lindi nikiwa mwalimu, nashangaa kuwepo hadi leo. -Mtazamo ni chanya, akionyesha kutokubaliana na hali ya elimu ilivyo sasa. -Ujumbe mfupi wa simu -Mume
2 . Asante kwa kuueleza umma nazani wataelewa tatizo letu huku Lindi
-Chanya -Simu -Mume
3. Tatizo ni maisha magumu na kipato duni kwa wananchi wa huku.
-Hali hii ipo pia Mkoa wa Mtwara jaribu kutembelea pia Ujumbe mfupi wa simu -Mume
Kifungu 2: Uhalisia wa Utendaji Kazi
Hitaji: Elezea kwa kifupi kazi ulizofanya kulingana na mpango kazi wako na mbinu za kiuandishi ulizotumia kufikia malengo.Tafadhali ambatanisha ratiba ya safari zako na watu uliozungumza nao na kuwahoji. ( Kiambatanisho)
Binafsi baada ya kufika eneo la uchunguzi (Mkoa wa Lindi) nilielekea kwenye ofisi za Chama cha Walimu (CWT) mkoani hapo nilifanya mahojiano na Katibu wa Mkoa Hassan Said ili kupata picha ya awali ya hali ya elimu mkoani hapo.
Niliamua kufanya hivyo maana CWT ni moja wa wadau muhimu wa elimu nchi nzima na pamoja na majukumu yao mengine wao huwa wawazi kwa kila suala linalohusiana na elimu iwe mafanikio ama vikwazo.
Baada ya mazungumzo na katibu huyo wa mkoa nililazimika pia kufanya mahojiano na makatibu pia wa wilaya ya Lindi Vijijini, Bw. Baltazar Lukanga na Bi. Angela Halla ambaye ni Katibu wa CWT halmashauri ya wilaya ya Lindi kabla ya kuyatembelea maeneo yao.
Baada ya kufanya mazungumzo na viongozi hao wa CWT nilienda moja kwa moja vijijini na kuanza kufanya mahojiano na baadhi ya walimu, wanafunzi, wananchi, viongozi pamoja na wakuu wa baadhi ya shule za msingi na sekondari kuhusiana na mada nzima.
Nilifanya hivyo huku nikijionea hali halisi ya suala nzima na kuangalia mbinu zinazofanyika katika kukabiliana na changamoto ambaozo ndio nyingi nimeziibua katika mada nzima.
Niliweza kutumia mbinu mbalimbali za kupata taarifa ikiwa ni pamoja na kufanya mijadala isiyo rasmi ya mazungumzo kuhusiana na uchunguzi, kufanya mahojiano na hata wakati mwingine kuhonga vitu vidogo kama pombe za asili na kisasa kutoa ofa za mlo (kama tupo kwenye mgahawa) sehemu ambapo kulikuwa na taarifa nzuri na wahusika kuonekana kutotoa ushirikiano.
Mara nilipomaliza ngazi zote za chini ndipo nilianza kufanya mazungumzo na viongozi wa serikali ngazi ya mkoa kuanzia sekta ya elimu na hadi utawala wenyewe wa eneo hilo.
Nilifanya mazungumzo na Kaimu Ofisa Tawala wa Mkoa, Abdul Dachi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa ambae alikuwa safarini Dar es Salaam kikazi. na Baadaye kufanya mazungumzo na Ofisa Elimu Mkoa, Jeseph Mnyikambi kabla ya kufanya kikao cha pamoja cha viongozi hao kupata taarifa za kina zaidi kuhusiana na elimu.
Licha ya kufanya mazungumzo na idadi kubwa kutokana na mazingira yenyewe yapo baadhi ya mazungumzo yalikuwa rasmi zaidi na hivyo kuchukua hadi majina ya wahusika, baadhi ya majina hayo ni kama ifuatavya:-
1) Abdul Dachi (Kaimu Ofisa Tawala Mkoa)
2) Joseph Mnyikambi (REO)
3) Salufu Kakama (Ofisa Elimu Taaluma Wilaya Ruangwa)
4)Mohamed Mtahu (Ofisa Elimu taaluma Lindi vijijini)
5) Baltazal Lukanga (Katibu CWT Wilaya Lindi vijijini)
6) Ally Hassan (Mkuu wa Nyangao Sec.)
7) Tupe Kayinga (Mkuu wa Ruangwa Sec.)
8) Shannel Nchimbi (Mkuu Nkowe Sec.)
9) Alli Mng’umba (Mkuu wa Lindi Sec.)
10) Angela Hala (Katibu CWT wilaya Lindi)
11) Badiru Shaweji (Walimu M/S)
12) Mohamed Mkota (Mwalimu M/S)
13) Somoe Chipinda (Mwalimu Mkuu Chilangalile)
14) Furaha Nyagali (Mwalimu)
15) Rehema Kihombo (Mwalimu)
16) Somoe Mohamed (Mwanafunzi)
17) Aini Rashid (Mwanafunzi)
18) Amandus Chitanda (Mwalimu)
19) Sylivesta Edwald (Mkazi wa Ruangwa)
20) Said Magombo (Mkazi wa Lindi)
21) Amina Ajabu (Mkazi wa Lindi)
22) Jeseph Mjahid (Mkazi wa Nyangao)
23) Adrian Abdallah (Mkazi Lindi vijijini)
24) Mwanaidi Said (Mwanafunzi)
25) Kasim Rashid (Mkazi wa Mnazi Mmoja)
26) Kulwa Tapa (Mkazi wa Mnazi Mmoja)
27) Merry Mtimbi (Mkazi wa kijiji cha Kibutuka)
28) Bahia Abubakar (Mkuu wa Sec. Kibutuka)
29) Athuman Chihua (Mkazi wa Lindi)
30) Juma Milanzi (Mkazi wa Lindi vijijini)
31) Salum Mwaya (Mwalimu)
Eneo la kazi na utaratibu wa siku Tarehe na siku zilizotumika
-Safari ya kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Lindi -24/04/2009
-Kufanya mazungumzo na mahojiano na wananchi wakazi wa pembezoni mwa Mji wa Lindi.
-25/04/2009, siku moja baada ya kuwasili mkoani hapo, nilifanya kazi hiyo kwa muda wa siku mbili.
-Nilitembelea baadhi ya shule za msingi na sekondari Lindi mjini pamoja na zile za wilayani kwa siku tofauti. -27/04/2009 mara baada ya uchunguzi wa awali nitatumia siku 2.
-Kufanya mahojiano na baadhi ya wazazi, viongozi wilayani Ruangwa na baadhi ya maeneo ya Lindi vijijini -29/04/2009 kazi hiyo niliifanywa kwa siku 3
-Siku hii nilianza safari ya kurudi Dar es Salaam. -01/05/2009 baada ya kumaliza.
Tafadhali eleza yaliyojiri wakati wa utekelezaji wa kazi.
Mambo gani ulifanikiwa na ulipata changamoto zipi?
Mara baada ya kumaliza kazi hii yapo mambo mengi ambayo nimeyabaini katika uchunguzi wote. Kwanza nimebaini kuwa mbali na kuwepo kwa mazingira magumu ya elimu mkoani Lindi, wazazi nao hawana mwamko wa elimu. Wengi wao hasa vijijini hawasamini elimu kabisa na wakati mwingine hawaoni umuhimu kwa kuigharamia ama kuirithisha kwa watoto.
Idadi kubwa ya wazazi hawakwenda shule kabisa au kupata elimu duni ambayo haikuwasaidia. Wengi hawapendi kujishughulisha ili kuingiza kipato cha ziada hali inayochangia kuwa na maisha duni. Mila kama za Jando na Unyago zinaiathiri jamii kutokana na kuona ni muhimu zaidi ya elimu hivyo mara nyingi mtoto anasitishwa masomo na kwenda kuchezwa porini muda wa mwenzi mmoja hadi miwili huku mtoto akikosa masomo.
Watoto wengine hutumika kufanya biashara ndogo ndogo za wazazi wao na kuingiza pato la familia na baadhi ya mabinti wa kike huachiwa majukumu wakati mwingine ya familia. Watoto wengi hulelewa na upande mmoja hasa mama au bibi baada ya mama kupata mimba zisizo tarajiwa.
Changamoto kubwa ilikuwa ushawishi wa kupata taarifa za ndani zaidi za jamii hali ambayo wakati mwingine nililazimika kutoa chochote kulingana na mazingira (ofa ya chakula pombe za kienyeji/kisasa bia) pengine fedha kidogo.
Kifungu 3: Mafunzo
Hitaji 1:
Matukio au tukio gani la mpango wa Jifunze kutoka TMF uliloshiriki:
• Mdahalo wa awali kwa wapewa ruzuku kabla ya habari (pre-story session)
• Mafunzo kazini kutoka kwa kocha (mentor)
• Mdahalo wa kutafakari baada ya kuandaa na kuchapisha habari (post-story session)
• Mafunzo ya muda mfupi , mafunzo kwa awamu,
• Darasa la utaalamu (master class)
Eleza kwa kifupi ulichojifunza kutokana na ushiriki wako katika mpango wa Jifunze:
Nimeongeza ujuzi kiasi fulani wa namna ya kufanya habari za uchunguzi mbali na mbinu za awali baada ya kupata mafunzo ya muda mfupi toka kwa wawezeshaji wa JIFUNZE. Hiyo ni baada ya kupata mafunzo hayo tumeshiriki katika kutoa michango na changamoto kwa washiriki wote ikiwa ni pamoja na kuelezwa namna ya kukabiliana nazo katika habari za uchunguzi.
Hitaji 2: Eleza utaalam na ujuzi uliopata katika kutimiza kazi yako.
1. Maandalizi:
o Ni kwa kiasi gani umeboresha ujuzi wako wa kuandaa mpango mkakati wa kazi ?
Umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana
Umeongezeka
umeongezeka kiasi
Haujaongezeka kabisa
o Kwa kiasi gani umeongeza ujuzi wako wa kukusanya habari? Kugundua na kufuatilia kwa uhakika vyanzo vyako vya habari)
Umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana
Umeongezeka
Umeongezeka kiasi
Haujaongezeka kabisa
Ukusanyaji wa Habari
• Kwa kiasi gani umeongeza uzoefu wako wa kufuatilia taarifa za mtandao na upembuzi yakinifu wa taarifa?
Umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana
Umeongezeka
Umeongezeka kiasi
Haujaongezeka kabisa
• Kwa kiasi gani umeboresha ujuzi wako wa kuhoji ili kupata taarifa zote muhimu kutoka kwa vyanzo vya habari?
Umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana
Umeongezeka
Umeongezeka kiasi
Haujaongezeka kabisa
• Kwa kiasi gani umeongeza uwezo wako wa kutambua na kubaini mambo wakati wa kukusanya habari?
Umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana
Umeongezeka
Umeongezeka kiasi
Haujaongezeka kabisa
o Uandishi wa habari / Uandaaji vipindi:
o Kwakiasi gani umeongeza ujuzi wako wa uandishi wa habari au uandaaji wa habari za matukio na vipindi?
Umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana
Umeongezeka
Umeongezeka kiasi
Haujaongezeka kabisa
3. Mengineyo, ……………………..
Programu ya TMF ni nzuri endapo itashirikia na vyombo vya habari kusaidia kutoa taarifa kama hizi, ambapo awali zilikuwa zikishindikana kupatikana kutokana na uwezo mdogo wa vyombo vya habari kugharamia wanahabari wake kutafuta taarifa kama hizi kwa baadhi ya sehemu hasa vijijini.
Kifungu 4: Matarajio/Nini kifanyike
Una maoni yoyote kwa TMF ?
Upo umuhimu wa kupunguza mlolongo wa masharti kabla ya muhusika kupata fungu la kufanya kazi ya wazo lake. Zipo taarifa za awali za uchunguzi ambazo zinakuwa na mwelekeo mzuri licha ya kutokuwa na maelezo na ufafanuzi wa kina ambazo endapo zitapewa sapoti zinaweza kuleta mabadiliko. TMF wakati mwingine mmekuwa mkizitia kapuni na kutaka taarifa za kina zaidi, swali ni kwamba endapo mtakuwa mkipata taarifa karibu asilimia 60 ya wazo husika mwandishi ataenda kufuata nini eneo la tukio. Hili liangaliwe. Bajeti ni finyu, mfano mzuri mimi nilikuwa Lindi nimelazimika kutumia kiasi cha ziada changu ili kukamilisha kazi yangu. Maeneo ya vijijini ni mbali na mtu unalazimika kukodi gari kiasi cha shilingi 40,000/- kwa siku kwenda na kurudi vijijini. Huku bajeti ya siku umepewa shilingi 50,000/- kwa kila kitu kula, kulala, kusafiri eneo la tukio, hii haitoshi na ni vema yakaangaliwa maeneo na hali halisi. Endapo kitu kama hicho hakita fanyika watu wenye moyo mdogo watakuwa wakiishia maeneo ya karibu na kushindwa kwenda sehemu za ndani vijijini ambapo nipo kwenye hali halisi tukio.
SEHEMU B: TAARIFA YA FEDHA
Tafadhali wasilisha TMF taarifa kuhusu uhalisia wa matumizi ya kifedha.
Tafadhali onyesha matumizi halisi.
Kifungu 1: Taarifa ya kifedha
Maelezo ya kifungu cha kazi iliyotumia fedha Gharama katika bajeti Gharama halisi iliyotumika Salio
Malipo ya posho kwa siku 9 eneo la kazi. 450,000/- 570,000/- –
Mawasiliano ya simu eneo la kazi na baada. 45000/- 48,000/- –
Usafiri Lindi mpaka Dar es Salaam siku mbili. 46,000/- 36,000/- 10,000/-
Gharama nyingine mtandao 20,000/- 35,000/- –
JUMLA 561,000/- 689,000/- -118000 (deni)
1Tafadhali husisha mrejesho uliopewa kwa njia ya mtandao (websites/blogs/forum)