Profesa Sospeter Muhongo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiingalia Taarifa hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakwanza kulia wakishuhudia tukio hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa madini mbalimbali uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mawaziri pamoja na Wabunge wakifatilia kwa makini uwasilishwaji wa Ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya kupokea Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya uchunguzi wa Mchanga wenye madini Ikulu jijini Dar es Salaam.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo kuanzia leo tarehe 24 Mei, 2017. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.
Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kupokea ripoti ya taarifa ya Kamati Maalum ya uchunguzi wa Mchanga wenye madini Ikulu iliobainisha uozo mkubwa hali iliyomlazimu kumfukuza kazi waziri huyo pamoja na watendaji wakuu katika wizara yake.